Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marioo , Paula wapanga kuwafunga watu midomo

Muktasari:

  • Marioo amesema atafunga ndoa na mzazi mwenzake hivi karibuni kwa mipango ya Mungu baada ya kumtakia heri ya kuzaliwa Paula.

BAADA ya mtoto, kuchumbiana, sasa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Omar Mwanga 'Marioo' amesema kinachofuata ni ndoa na Paula Kajala na mashabiki wasiwe na wasiwasi.

Marioo amesema atafunga ndoa na mzazi mwenzake hivi karibuni kwa mipango ya Mungu baada ya kumtakia heri ya kuzaliwa Paula.

Kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Marioo aliandika; "Happy Birthday Love of My Life ❤️ @therealpaulahkajala You know I love you so much & Nashukuru kwa Namna ambavyo Umechagua Mimi Kuwa Mume kwako & Baba. NITAKUPENDA NA KUKUHESHIMU SIKU ZOTE ❤️🌹".

Mwanaspoti lilimtafuta Marioo na kupiga naye stori na kuhusu ndoa alisema; “Muda si mrefu mambo yatakuwa mazuri, tulikuwa tunaendelea kujuana, nadhani sasa tunafahamiana vizuri, hivyo watu wasiwe na shaka, tutafunga ndoa muda si mrefu."

“Hatujui labda kuchelewa kwetu kuna kitu Mungu amekiepusha, siku zote haraka haraka haina Baraka,” amesisitiza Marioo ambaye wamejaaliwa kupata mtoto mmoja na Paula.

Aidha Marioo amezidi kuweka wazi kwa Mwanapoti, kwenye mahusiano yake haya  mapya alimuomba Mungu apate mwanamke ambaye sio mwenye tamaa wala mambo mengi na kwa hilo amefanikiwa.

Kwa upande wa Paula ameliambia Mwanaspoti; "Unajua kila jambo na wakati wake, yamesemwa mengi juu yangu lakini nashukuru Mungu siku si nyingi nitaandika historia katika maisha yangu, kwa lugha nyingine, naolewa ‘soon’ kwani nishatambulishwa kwa wakwe zangu,” amesema Paula.