Marioo awataka vijana kuwa karibu na mitandao

MSANII wa muziki wa Bongofleva, Omary Mwanga ‘Marioo’ anayetamba kwa sasa nchini amewataka vijana wawe karibu na mitandao ya kijamii kutokana na kuwa na fursa nyingi.
Marioo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la Infinix note 30, note 30 pro na note 30 vip uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Marioo ambaye ni balozi wa Infinix note 30, amesema vijana wawe karibu na mitandao ya kampuni hiyo kwani fursa nyingi.
“Kuna shindano la vijana la kuibua vipaji linalojlikana kama Star Alliance ni zuri kwao na watalipata kupitia mitandao ya kijamii,”
Marioo akizungumzia upande wa huduma ya simu hizo amesema kuunganishwa na simu hiyo akiwa na simu hiyo anafanya kazi nyingi.
“Kuunganishwa na hii simu nikiwa kama kijana mwenye kazi nyingi za kufanya pasipo kupoteza muda, Infinix NOTE Series imekuwa suluhisho kwangu kwa pande zote, fikiria inachukua dakika 30 tu nishati ya betri kufikia asilimia 80, lakini pia inaniruhusu kucheza michezo wakati simu ikiendelea kujaa chaji, kuchajisha simu nyengine, licha ya kuwa na sifa hizi zote zaidi ninavutiwa na gharama yake ni rahisi kila kijana anaweza kukifikia na kutimiza malengo yake kupitia teknolojia,”

Upande wa Ofisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Kurupa amesema;”Tupo kwa lengo la kila mtanzania kuweza kutumia simu janja na ndio maana bei zetu ni nafuu.”