Manara, Zaiylissa mahaba kama yote

Muktasari:

  • Haji Manara na Zaiylissa Jumatatu Aprili 15 walionekana pamoja ndani ya gari hadi wakishuka kwenda kusaini dili la ubalozi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha na Manara ndiye aliyeenda kusaini.

ZILE habari za kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikidai kuwa Haji Manara na mke wake muigizaji Zaiylissa ndoa yao imevunjika basi jua kwao ndio kwanza mahaba kama yote.

Haji Manara na Zaiylissa Jumatatu Aprili 15 walionekana pamoja ndani ya gari hadi wakishuka kwenda kusaini dili la ubalozi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha na Manara ndiye aliyeenda kusaini.

Kitendo hicho pamoja na mahaba waliokuwa wakionyeshana kabla na baada ya kuingia kwenye hafla hiyo wakionekana pia kuwa na furaha kinafuta uvumi wa wawili hao wameachana zaidi ya mwezi na Zai karudi kwa wazazi wake.

“Jamani kweli mapenzi ni kitu cha ajabu, hawa Haji Manara na Zaiylissa habari zilisambaa kila kona ya jiji na mitandao ya ki-jamii wameachana na Zai amerudi nyumbani kwao huku Haji akibaki mpweke nyumbani kwake kwa mara nyingine, leo hapa tunashuhudia kitu tofauti,” alisema dada mmoja ambaye alikuwepo katika tukio hilo la Haji kupewa ubalozi.

Tangu uvumi uzagae wameachana, Zaiylissa hakuonekana kwenye mashindano ya kusoma Quran ya watu maarufu yaliyoandaliwa na Haji Manara Foundation na Mboni Show yaliyofanyika Serena Hotel na kuzidisha uvumi huo.

Hata hivyo, Sikukuu ya Eid, Aprili 10, 2023, wawili hao walionekana pamoja nyumbani kwa Manara na baadhi wakidai hawajaachana na wengine waliachana na wameombana msamaha na kurudiana.

Hata hivyo, Mwanaspoti limezungumza na Zaiylissa kuhusu habari za kuachana na mume wake na kufunguka hawajaachana bali kuna baadhi ya watu asilimia kubwa wanataka waachane na hajui kwa nini wanakuwa hivyo na Kutoonekana pamoja kila mahali haimaanishi wameachana na kukiri ameona hayo kwenye mitandao ya kijamii.

"Hizi habari mimi nimeanza kuziona kwenye mitandao ya kijamii nimesoma na kukaa kimya sababu ukweli nauju mimi mwenyewe kwanza hata kama mimi nikiachana na Manara ndio nitakuwa mimi wa kwanza jamani? kiufupi mimi niko na mume wangu Haji na sio kila anapokuwa yeye na mimi basi niwepo jamani tutakuwa basi hatufanyi shughuli zingine basi, ila najua watu asilimia kubwa wanatamani tuachane," alisema Zaiylissa

Kwa upande wa Manara simu yake ilikuwa inaita bila ya kupokelewa lakini juzi Jumatatu kwenye akaunti yake ya Instagram baada ya kutoka kwenye hafla hiyo ya kusaini dili la ubalozi aliandika; "Toka nimemuoa mke wangu, leo for the first time nakuwa peke yangu bila kipenzi changu Zai; Pangani, Are You Ready?; Am here baby.... @jumaa_aweso umejiandaa ?

Kisha Zai akajibu kwenye ujumbe huo; "I miss you already Mume wangu...Meboreka."