Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama wa Miss Universe 2025 atoa somo kwa wazazi

MAMA Pict

Muktasari:

  • Lulu ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo,  Agosti 24, 2025 kwenye Ukunbi wa The Superdome, Masaki ilipokuwa inafanyika fainali ya mashindano hayo ambapo binti yake ameibuka mshindi na kuzawadiwa gari aina ya Hyundai Creta na pesa Sh10 milioni.

LULU Makoi, Mama mzazi wa mshindi wa Taji la Miss Universe Tanzania 2025, Naisae Yona, ametoa wito kwa wazazi kusapoti talanta za watoto wao badala ya kuzikandamiza.

Lulu ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo,  Agosti 24, 2025 kwenye Ukunbi wa The Superdome, Masaki ilipokuwa inafanyika fainali ya mashindano hayo ambapo binti yake ameibuka mshindi na kuzawadiwa gari aina ya Hyundai Creta na pesa Sh10 milioni.

"Kwa wazazi napenda kusema wawe karibu na watoto wao, wawasikilize vitu vingine vinaweza kuja kama vya kijinga kwa sababu labda pengine wapo mashuleni. Lakini ndoto za watoto zisikandamizwe wazibebe na kuendelea kuwashauri wakati sahihi jambo litakua," amesema Lulu.

Mama huyo amesema, binti yake ameishi ndoto hiyo inayohusu urembo tangu akiwa Shule ya Sekondari huko Cape Town, Afrika Kusini lakini alimzuia kutokana umri mdogo aliokuwa nao kipindi hicho.

"Ameishi na vitu vingi tangu akiwa Shule ya sekondari huko Cape Town, Afrika Kusini na alikuwa anatamani sana kufanya, lakini nilimzuia mara nyingi kujihusisha na vitu hivi kabla ya umri wa kujitambua. Lilipofika mashindano haya aliomba na akasema anajitambua naomba nikashiriki nikamwambia nitakupa sapoti yangu kwa asilimia mia moja," amesema Lulu.