Malkia Karen kumuitisha Gardner Babu soon!

Monday August 02 2021
kareen pic
By Nasra Abdallah

MASTAA hawataki utani buana katika suala la kuitwa mama. Hii ni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, wengi wao walionekana kujikita zaidi katika kula bata na kuona kama kuzaa mapema utapitwa na wakati.

Lakini hali kwa sasa imebadilika kwani wengi wao wanaitwa mama huku wengine wakiwa mbioni kuitwa mama akiwemo Malkia Karen.

Hii ni baada ya Mwanaspoti kumshuhudia msanii huyo tumbo lake likiwa na mabadiliko ikionyesha ana ujauzito.

Siku hiyo msanii huyo aliyekuwa kavaa Fulana, taiti fupi na kipochi cha kiunoni alionekana akihangaika kuficha tumbo lake , lakini ndio hivyo waswahili wanasema pembe la ng’ombe halifichiki.

Hata Mwanaspoti baada ya kushtukia ishu hiyo na kumpa hongera kwa hatua yake hiyo, majibu yake yalikuwa “Hongera ya nini dada, hamna kitu bana, nimetegea tu kufanya mazoezi na siku hizi ninakula sana,”.

Alipoulizwa mbona na midomo inaonekana kumkauka na kupaka mafuta maalum kwa ajili ya kuulainisha mara kwa mara, alisema hiyo ni kawaida yake na pia sasa hiki ni kipindi cha baridi hivyo hali hiyo humtokea mara kwa mara.

Advertisement

Tangu aachie wimbo wake wa ‘Lawama’ mwaka 2018 ameendealea kufanya vizuri sokoni.

Tofauti na wasanii wengine ambao huwachukua muda kujulikana katika tasnia hiyo, kwake imekuwa rahisi huku wadau wa burudani wakisema imechagizwa zaidi na umaarufu alionao baba yake Gardner G Habash, ambaye ni mtangazaji maarufu hapa nchini.

Vibao ambavyo hadi sasa ameviachia ni pamoja na Tunaendanda, Lawama, Washa, Tabu, Sina, Shada na vingine.

Advertisement