Luizer Mbutu wa Twanga Pepeta Mwenyekiti mpya Chamudata

Dar es Salaam. Mwanamuziki kutoka bendi Twanga Pepeta,Luizer Mbutu,amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya,chama cha wanamuziki wa dansi Tanzania(Chamudata).

Luizer alitangazwa kushinda nafasi hiyo leo Jumatano Mei 11,2022,na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi,Jamal Rwambow katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika  jijini humo.

Katika nafasi hiyo Luizer alipata  kura 97 akiwaacha washindani wake kwa mbali akiwemo Muumini Mwinjuma aliyepata kura 37 wakati nafasi ya tatu alishika Said Kaunga aliyepata kura 35 .

Nafasi ingine iliyokuwa ikigombewa ni ya Katibu Mkuu,ambapo mshindi ni Said Kibiriti aliyeshinda kwa kupata kura 131 akimshinda mshindani wake aliyekuwa akitetea nafasi hiyo,Hassan Msumari aliyepata kura 35.
Nafasi zingine zilizogombewa na washindi kwenye mabano ni Makamu Mwenyekiti(Abdallah Hemba) na Katibu Msaidizi Baraka Selus ambaye hakuwa na mshindani katika kinyang'anyiro hicho.

Wakati kwa upande wa wajumbe sita wa kamati tendaji waliopenya ni  Said  Mdoe,Bernedict Sanga, Gabriel Bakilana,Cecy Jeremiah Lugome,Rhobi Abubakari Chacha na  Abbu Omar Abubabar