Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusah aikana ndoa ya Aunty Ezekiel

Kusah Pict

Muktasari:

  • Kusah ameliambia Mwanaspoti hivi karibuni, aliamua kuongea vile, wamefunga ndoa na Aunt Ezekiel sababu yalikuwa maswali mengi juu ya zile picha, ila ukweli, wawili hao hawajawahi kuoana.

KAMA unakumbuka Oktoba 28, 2021 kwenye pati ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwigizaji wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel, mkali wa Bongo Fleva, Salmin Issa 'Kusah' alikaririwa wamefunga ndoa na mzazi mwenzie huyo baada ya kusambaa kwa picha zilizoonyesha wamevaa mavazi ya ndoa, sasa amekuja kivingine kwa kukanusha kuwa hajawahi kumuoa.

Kusah ameliambia Mwanaspoti hivi karibuni, aliamua kuongea vile, wamefunga ndoa na Aunt Ezekiel sababu yalikuwa maswali mengi juu ya zile picha, ila ukweli, wawili hao hawajawahi kuoana.

"Kuoa ni suala la kheri, ila leo acha niseme ukweli, sijamuoa Aunt Ezekiel, kipindi kile niliongea tu kufurahisha watu na baada ya kupata simu nyingi za maswali kuhusu kama tumefunga ndoa, zile picha ilikuwa ni promo ya wimbo wangu 'I Wish', mimi ningeoa ungeona tu mtikisiko wa mji (anacheka)," alisema Kusah.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilipomuuliza mipamgo ya ndoa na mwanadada huyo aliyewahi kutamba katika mashindano ya Urembo nchini, Kusah alisema huenda mwaka 2025 hautamalizika kabla ya kutekeleza jambo hilo, kwani anaona ni muda mwafaka kufanya hivyo.

"Daah hii sio masihara, mwaka huu lazima nimuoe dada wa watu jamani, yaani hadi namuonea huruma aisee kwa uvumilivu alionao wa kusubiri ndoa, hii sasa nasema ukweli kutoka moyoni kuwa mwaka huu hautaisha namuoa Aunt Ezekiel na nampenda sana," alisema Kusah.

Aunt na Kusah walianza kuwa wapenzi baada ya mwanadada huyo kutengana na mzazi mwenzie mwingine, Mose Iyoboe ambaye ni dansa wa Diamond Platnumz, wakati Kusah naye alikuwa ametoka kutengana na mzazi mwenzie ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya pia, Ruby.