Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mose Iyobo ashindwa kulikwepa jina la Aunt Ezekiel

Muktasari:

  • Licha ya wawili hao kuachana muda mrefu na kila mmoja kuendelea na maisha yake, jina la Aunt bado limeendelea kuwa sehemu ya mazungumzo mengi yanayomhusu dansa huyo.

KAMA kuna jambo ambalo limekuwa likijirudia kila Mose Iyobo anapoketi kufanya mahojiano, basi ni kurejea kwa jina la mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel.

Licha ya wawili hao kuachana muda mrefu na kila mmoja kuendelea na maisha yake, jina la Aunt bado limeendelea kuwa sehemu ya mazungumzo mengi yanayomhusu dansa huyo.

Kwa sasa Mose yupo kwenye mahusiano na mwanamitandao Masha Love, huku Aunt naye akiwa na maisha yake. Hata hivyo, kila Mose anapozungumza na vyombo vya habari, mara nyingi hujikuta akijibu maswali yanayohusu mtoto wao, mahusiano yao kama wazazi wenza au kauli zinazotolewa na mzazi mwenzake.

Hivi karibuni, Mose alijikuta tena akizungumzia suala hilo baada ya kuibuka kwa mvutano mwingine wa maneno kati yake na Aunt kuhusu malezi ya mtoto wao. Akizungumza na Mwanaspoti, dansa huyo amesema hana shida kujibu maswali yanayomhusu mwanaye kwa sababu anaamini ni haki yake kama baba.

"Mimi sitaacha kumuongelea mwanangu sehemu yoyote kwani nina haki naye, kikubwa simzungumzii mama yake, nazungumzia mtoto damu yangu," amesema Mose.

Mose aliweka wazi kuwa haoni sababu ya kuzuiwa kujibu maswali kuhusu mtoto wake kwa kigezo cha kutokuwa na mawasiliano mazuri na mama wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wake, anapoulizwa kuhusu mtoto wake ataendelea kujibu kwa sababu ni sehemu ya maisha yake kama mzazi.

Licha ya kuwa kwenye ukurasa mpya wa maisha yake akiwa na Masha Love, jambo moja linaonekana kubaki wazi; jina la Aunt Ezekiel bado haliko mbali na mahojiano ya Mose Iyobo. Iwe ni kwa sababu ya malezi ya mtoto wao, historia yao ya pamoja au mijadala inayozuka mara kwa mara, simulizi ya wawili hao inaendelea kuwa moja ya zinazovuta hisia katika ulimwengu wa burudani.