Kusah afichua ndoto ya kumuoa Ruby
Muktasari:
- Kusah ambaye amepata mtoto mmoja na Ruby ndoto yake ya kumuoa ilizimika na aliwahi kusema watafunga ndoa, kabla ya kuachana na kwa sasa yupo kwenye penzi la Aunty Ezekiel.
Msanii wa Bongo Fleva, Kusah amesema kuzaa na mwanamke haina maana ni lazima amuoe, baada ya kuulizwa endapo alikuwa na mipango ya kumuoa mpenzi wake wa zamani, Ruby kabla ya kuachana.
Kusah ambaye amepata mtoto mmoja na Ruby ndoto yake ya kumuoa ilizimika na aliwahi kusema watafunga ndoa, kabla ya kuachana na kwa sasa yupo kwenye penzi la Aunty Ezekiel.
"Siwezi kusema hatukuwa tumeendana na Ruby ndiyo maana sikumuoa, hapana, ila siyo lazima ukizaa na mwanamke ndiyo uje umuoe. Hata kama niliwahi kusema tutafunga naye ndoa, yawezekana mipango iliharibika kabla ya kufikia lengo hilo hivyo tukabaki kuwa wazazi ambao tunaheshimiana na uzuri kila mmoja ana mahusiano yake mengine kwa sasa. Ndiyo maana nimesema mnaweza tu mkazaa na mwishowe kila mtu akaendelea na mambo yake na hiyo desturi siyo ya kwangu peke yangu ipo dunia nzima."
Kusah ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo na ndiye aliyemwandikia pia Ruby wimbo wa Ntande na Alele, amewahi kutamba na nyimbo kama I wish, Nilewe, Nakupenda, I don't Care, Hujanikomoa na nyingine nyingi.
Hivi karibuni alizindua EP yake 'Bumbuli Boy' ikimaanisha nyumbani kwao Bumbuli mkoani Tanga. Pia amefichua ameshamuoa Aunty kimya kimya muda mrefu.