Kundi la P-Square kurejea?

Thursday November 18 2021
p pic
By Nasra Abdallah

Kundi la P-Square kurejea? hayo ndio maswali watu wanajiuliza kwa sasa baada ya wasanii wanaounda kundi hilo, Paul na Peter Okoye kuonekana tena pamoja.
Hii ni baada ya jana Jumatano Novemba 18, 2021 wawili hao kuonekana kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika makutano yao hayo, Paul alionekana akiingia ndani ya nyumba ya kifahari na kumfuata pacha wake Peter kisha kumkumbatia huku akiwa anamshagaa.

p pic 1


Pia wapambe waliokuwa nao walionekana wakifurahishwa na kitendo hiko huku wengine wakisikika wakitaja jina la familia yao la  Okoye.
Ikumbukwe kundi hilo kabla ya kuvunjika kwake mwaka 2015, lilijizolea umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali ikiwemo Beautiful Onyinye, Temptation, No One Like You na nyingine nyingi.
Chanzo cha kutengana kwao kulisababishwa na malalamiko kutoka kwa Peter aliyetaka mabadiliko katika uongozi, kwa kuwa uliokuwepo wa kaka yao Jude aliuona umekaa kifamilia zaidi kuliko kibiashara.
Aidha  jambo hili mwenzake Paul hakuliafiki na hapo ndipo kikawa chanzo cha kundi hilo kuvunjika na kila mtu aliamua kufanya kazi kivyake ambapo Paul alianza kutumia jina la Rudeboy na kuaanzisha record label yake ya ‘Rudeboy’ huku  Peter yeye akijipa jina la  Mr P naye alitangaza uongozi wake mpya.

Advertisement