Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Konshens aachia kichupa cha Shake It

Muktasari:

  • Konshens ndiye anayeongoza nyimbo nyingi kubwa zaidi za Dancehall za muda wote duniani, safari hii anajidhihirisha kuwa mkali wa miondoko hiyo.

MSANII maarufu wa kimataifa wa Jamaica, Konshens, ameachia wimbo mpya uitwao ‘Shake It’ ukiwa katika audio na video.

Konshens ndiye anayeongoza nyimbo nyingi kubwa zaidi za Dancehall za muda wote duniani, safari hii anajidhihirisha kuwa mkali wa miondoko hiyo.

Kibao hicho kimetayarishwa na prodyuza mkali, Costa Rica BomboCat, ambapo Konshens anaonyesha umwamba katika muziki wa Afro Latin.

Akizungumzia wimbo huo, Konshens amesema: "Hii inaashiria kurudi kwa Dancehall, ni muziki ninaoupenda kuliko kawaida. Ni haki yangu sasa kuhakikisha nawafurahisha pia mashabiki zangu.”

Konshens anaimba kwa hisia, uchangamfu na kutawala jukwaa katika uwezo wa hali ya juu sana.

“Nilipata beat nikiwa Kenya mwaka mmoja uliopita. Nilianzisha studio yangu kwenye simu yangu tu na kurekodi nikiwa hotelini, Nairobi, Kenya," amesema na kuongeza;

"Pamoja na kelele nyingi zilizonizunguka, niliitawalisha akili yangu kwenye kurekodi wimbo wangu huo.”

Konshens anazo nyimbo kadhaa zilizotangulia kabla ya huu, kwa uchache ni pamoja na ’Bruk Off Yuh Back’, ‘Turn Me On’ na ‘Gal a Bubble’.