Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kuachika, JLO ataka kujiua

Muktasari:

  • JLO aliyasema hayo kwenye tamasha lake la UP All Night lililofanyika Las Vegas akisema kipindi hicho kilikuwa kigumu kwenye maisha yake.

MWANAMUZIKI wa Marekani, Jennifer Lopez (JLO) amesema aliwahi kufikia hatua ya kutaka kujiua baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Marc Anthony mwaka 2014.

JLO aliyasema hayo kwenye tamasha lake la UP All Night lililofanyika Las Vegas akisema kipindi hicho kilikuwa kigumu kwenye maisha yake.

Staa huyo wa kibao cha 'Waiting for Tonight' alisema alijikuta akibeba majukumu mazito kama mama ya kulea watoto mapacha peke yake Max Muñiz na Emme Muñiz, aliozaa na mumewe huyo.

"Nilikaribia sana kukata tamaa na kila kitu katika maisha yangu hadi kufikia hatua ya kujiua,” alisema Lopez.

Alisema mtu pekee aliyemsaidia kutoka kwenye haliu hiyo ni mshauri wa maendeleo binafsi marehemu Louise Hay, ushauri uliomsaidia kubadili mawazo hayo mabaya.

Kwa mujibu wa Lopez, Hay “Aliniuliza kama mimi ni mchezaji wa dansi, nikamwambia ndiyo kisha akaniuliza, unapojifunza dansi na ukakosea hatua inayofuata unafanya nini? nikamjibu naendelea kucheza.

Mwimbaji huyo alisema mwandishi huyo alimjenga na kumuweka sawa kisaikolojia na kumueleza haijalishi anapitia nini, muhimu ni kuendelea kusonga mbele bila kukata tamaa.

“Nawatakia ninyi nyote kitu hicho hicho, haijalishi maisha yanakuletea changamoto gani, endeleeni kucheza, kucheza na kupambana tena.”