Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala, Harmonize wazua utata mpya

KAJALA Pict

Muktasari:

  • Jina hilo la Kiislamu limezua tafsiri tofauti, huku wengi wakiamini linaweza kuwa ishara ya maandalizi ya ndoa yao inayotarajiwa kufungwa ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.

KWA sasa mashabiki na wapenzi wa filamu wanajiuliza juu ya Kajala Masanja, baadhi yao wakihoji kama kweli kimwana huyo amebadili dini kwa lengo la kutaka kufunga ndoa na Harmonize, hasa baada ya kuitwa mara kadhaa na 'baby' wake huyo jina la 'Swalha'.

Jina hilo la Kiislamu limezua tafsiri tofauti, huku wengi wakiamini linaweza kuwa ishara ya maandalizi ya ndoa yao inayotarajiwa kufungwa ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.

Mashabiki wengi wamekuwa wakihoji kama Kajala, anayejulikana kuwa ni muumini wa dini ya Kikristo, yuko tayari kubadili dini ili kuingia kwenye ndoa hiyo, wengine wamekuwa wakisema huenda ni uamuzi mkubwa unaohitaji muda, huku wengine wakiamini upendo unaweza kubadilisha mambo mengi.

Hadi sasa, Kajala hajatoa kauli rasmi kuhusu suala hilo, jambo linalozidi kuongeza mjadala.

Akizungumzia suala hilo na ukaribu wao katika kipindi hiki cha Ramadhani, Harmonize aliweka wazi kuwa mambo mengi yanayoonekana mitandaoni hayapaswi kutafsiriwa moja kwa moja.

"Kwanza watu wanapaswa kuelewa sio kila kitu kinachokuwa mitandaoni kina maana ile wanayofikiria, kumuita Swalha ni sehemu ya ukaribu wetu, lakini mambo mengine yanahitaji muda na uamuzi wa busara," amesema Harmonize.

Msanii huyo pia alithibitisha kuwa ndoa ipo kwenye mipango na inaweza kufungwa ndani ya mwezi huu, jambo linaloendelea kuvuta hisia za mashabiki wake.

"Ndoa ni jambo zuri, na kila mwanaume anatamani kufika hatua hiyo, mimi niko tayari na kama mipango itakamilika, basi ndoa itafungwa mwezi huu kama Mungu akipenda," amesema Konde Boy.

Katika kipindi hiki cha Ramadhani, Harmonize na Kajala wameonekana mara kadhaa wakiwa pamoja, wakialikwa katika futari na hata kupostiana picha zao mitandaoni.

Hata hivyo, Harmonize aliwahi kueleza kuwa ukaribu wao haupaswi kupewa tafsiri ya haraka.

"Watu wanaona picha wanahisi tayari kila kitu kimekamilika, lakini ukweli ni kwamba tunaheshimiana na tunakutana kama marafiki na watu wenye ukaribu maalumu kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu," amesema.

Kauli hizo zimeendelea kuchochea mjadala, huku baadhi ya mashabiki wakisema wazi kuwa wanaunga mkono ndoa hiyo na wako tayari kuona wawili hao wakianza maisha mapya, wengine, hata hivyo, wameendelea kuhoji kuhusu suala la dini, wakitaka kujua kama Kajala yuko tayari kwa mabadiliko hayo makubwa ya Maisha.

Licha ya maswali hayo, Harmonize amesisitiza kuwa jambo la msingi kwake ni furaha na maelewano kati yao.

"Kikubwa ni amani na furaha. Watu wataongea sana, lakini mwisho wa yote uamuzi ni wetu na tunaangalia kile kinachotufaa sisi na kipenzi changu," amesema.

Ukaribu wa Harmonize na Kajala unaendelea kuwa gumzo kubwa, hasa katika mwezi huu wa Ramadhani, huku mashabiki wakisubiri kuona kama kweli ndoa hiyo itafungwa kama alivyosema Harmonize na kama Kajala atachukua hatua ya kubadili dini au kubaki na imani yake ya sasa.

Mwanaspoti lilimtafuta Kajala kuhusu suala la kufunga ndoa na kama atabadili dini, amesema: "Niko mazoezini kipenzi, nitakupigia, ila sasa kwanini tusifunge ndoa? Suala la dini embu niache kwanza, subiri ndoa utapata majibu."