Jeje washika namba moja barani Afrika

Muktasari:

Wimbo huo uliotoka Februari 26, mwaka 2020, umeimbwa na msanii Diamond Platnumz ambapo hadi kufika leo Jumatano Januari 6, 2021 umeshatazamwa zaidi ya mara milioni 41.6.

Video ya wimbo wa Jeje  umeshika namba moja katika nyimbo zilizotazamwa zaidi barani Afrika mwaka 2020.
Wimbo huo uliotoka Februari 26, mwaka 2010, umeimbwa na msanii Diamond Platnumz ambapo hadi kufika leo Jumatano Januari 6, 2021 umeshatazamwa zaidi ya mara milioni 41.6.
Ni kutokana na watazamaji hao, taarifa iliyotolewa na mtandao huo wa YouTube juzi uliitaja kama wimbo namba moja kutazamwa barani Afrika.
Jeje umefuatiwa na wimbo wa  Duduke wa Simi msanii kutoka nchini Nigeria uliotazamwa mara milioni 29.
Namba tatu inashikwa na wimbo wa Waah! alioimba Diamond akimshirikisha msanii kutoka nchini DRC Kongo, Koffi Olomide iliyotazamwa mara milioni 25.1
Namba nne inakamatwa na wimbo wa Nobody ulioimbwa na DJ Nepture akiwashirikisha Joeboy wa Nigeria , Mr Eazi wa Ghana uliozamwa mara milioni 25.
Vibration wimbo ulioimbwa na Fireboy DML wa nchini Nigeria unashika namba tano kwa kutazamwa mara milioni 23.2, namba sita inakamatwa na Rayvanny kupitia wimbo wake wa Teamo uliotazamwa mara milioni 22.4.
Wimbo wa Gere ulioimbwa na Tanasha Donna akimshirikisha msanii Diamond umeshika nafasi ya saba ambapo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagrm, Tanasha hakusita kumshukuru Diamond.
 “Asante kubwa! Gere peke yangu na Baba Naseeb junior kuwa nyimbo za Kiafrika zilizotazamwa zaidi kwenye Youtube 2020.
“NinamshukuruDiamond Platnumz kwa kuniamini na kushirikiana nami kwa sauti kubwa na kwa wafuasi ambao wameniunga mkono na wanaendelea kuniamini hadi sasa. Shangwe kwa 2021 Inshallah kubwa. Ndoto inaendelea,”ameandika Tanasha.
Namba nane upo wimbo wa Dusuma ulioimbwa na Otile Brown na Meddy wa nchini Kenya uliotazamwa mara milioni 19 na namba tisa  inashikwa na wimbo wa  Olandi ulioimbwa na Innos B ambao umetazamwa mara milioni 17.9 n namba kumi inashikiliwa na Yemi Alade kupitia wimbo wake wa Shekere uliotazamwa mara milioni 16.4.