Jacqueline Wolper atamba hawezi kuachika

Muktasari:
- Wolper aliliambia Mwanaspoti kwa sasa wanakaribia kutimiza miaka mitatu na mume wake Rich Mitindo na kwa jinsi walivyo hana jeuri ya kumpa talaka au kumuacha.
MWIGIZAJI mkongwe wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema licha ya wengi kuizungumzia ndoa yake vibaya kwa lengo la kuivunja, haamini kama hilo linaweza kutokea.
Wolper aliliambia Mwanaspoti kwa sasa wanakaribia kutimiza miaka mitatu na mume wake Rich Mitindo na kwa jinsi walivyo hana jeuri ya kumpa talaka au kumuacha.
“Ni hivi wacha waongee tu vitu wasivyovijua, lakini hayo maneno hayawezi kumfanya mume wangu aniache kwa sababu jeuri hiyo hana na wala mimi siwezi kumuacha kwa namna yoyote ile,” alisema Wolper.
Wolper aliyasema hayo baada ya kuibuka maneno kutokana na kitendo cha yeye kuongea na Harmonize kwa muda mrefu katika sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wa Paula na Marioo na video ya wawili hao iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii ili Rich aione kwa lengo la kuvuruga ndoa yake, lakini anasema wanajisumbua kwani hilo haliwezi kutokea na mumewe hana jeuri hiyo.