Jacqueline Wolper aanza kugomea pete za uchumba

Muktasari:
- Wolper alisema ameakua kufanya hivyo kutokana na wanaume wengi kutoa ahadi ya ndoa na kisha kuingia mitini, jambo ambalo hataki limtokee kwa sasa.
NYOTA wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper, amegomea kuvishwa pete ya uchumba kutoka kwa mwanaume yeyote anayetaka kumchukua jumla akimtaka kwanza amalize utaratibu wote za kufunga ndoa ndipo zoezi la pete lifuate.
Wolper alisema ameakua kufanya hivyo kutokana na wanaume wengi kutoa ahadi ya ndoa na kisha kuingia mitini, jambo ambalo hataki limtokee kwa sasa.
Alisisitiza kuwa hataki tena kuvishwa pete na mwanaume bila ya kujiridhisha kwa kukamilisha kwa kufuata utaratibu wa hatua tatu ambazo ni utambulisho, kuvishwa Pete na ndoa.Aidha Wolper alisema, kwa sasa akipata mwanaume na wakaridhiana kuoana, itabidi mwanaume huyo afuate utaratibu anaoutaka na siyo kupeleka mambo kienyeji.
“Kwa sasa sitaki kuchezewa akili tena, nikipata mwanaume ajiandae kufanya vitu vitatu kwa wakati mmoja, yaani kunitambulisha, kunivisha pete na kunioa.
Kwa sasa sitaki kuvishwa pete halafu malengo hayatimii, nimeshaona ni ubabaishaji tu wa baadhi ya wanaume,” alisema Wolper.
Wolper aliwahi kuvishwa pete za uchumba na Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ambaye ni mfanyabiashara, Gee Modo nae ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya viatu na nguo maeneo ya Kinondoni jijini Dar lakini wote wakaingia mitini.
Wengine ni Jimmy Mgaya ni ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini na Mwami Rajabu ambaye ni mfanyabiashara wa madini raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.