Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Flora Mbasha afunguka ishu ya ndoa, kubadili jina

MBASHA Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti lilimtafuta Flora ambaye baada ya kuachana na aliyewahi kuwa mume wake, Emmanuel Mbasha aliolewa na Daudi Kusweka na kwa sasa kuna tetesi za kuachana naye na kuamua pia kubadili jina  na kuitwa Flora Mayala.

YAPO mengi yanayozungumzwa kuhusu msanii maarufu wa nyimbo za injili, Flora Mayala. Mengine yana ukweli lakini yapo ambayo ni uzushi.

Mwanaspoti lilimtafuta Flora ambaye baada ya kuachana na aliyewahi kuwa mume wake, Emmanuel Mbasha aliolewa na Daudi Kusweka na kwa sasa kuna tetesi za kuachana naye na kuamua pia kubadili jina  na kuitwa Flora Mayala.

Msikie Flora; “Mimi sijabadili jina kwa sababu ya kuachana na Daudi Kusweka, bali  nimeamua kutumia jina la baba yangu, jina la Mayala ni la baba yangu na sina  mpango wa kubadili tena jina, nitakuwa naitwa hivi hivi Flora Mayala hata itokee nini.”

“Na kuhusu habari za mimi kuachika kwenye ndoa, siko tayari kulizungumzia hili zaidi ya kazi zangu za sanaa, nimetoa nyimbo nyingi mpya na nzuri naomba wazifatilie kwenye ‘digital platform’ zote watazipata, ila niwaambie watu wasisahau kusali na kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema Flora.

Aidha Mwanaspoti lilimuuliza Flora kitu anachofanya aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha, kwa kusambaza habari zake kwenye akaunti yake ya Instagram, ameachana na Kusekwa  huku akidai anafanya siri watu wasijue na hiyo ni ndoa yake ya nne kuachika, alisema haya:

“Kunyamaza pia ni hekima, Mungu abariki kwa kila kitu na neema ya Yesu yatosha na ukishajua maisha ni darasa basi kubali kujifunza, sina cha kuzungumza zaidi ya haya,” alisema.

Flora kwenye akaunti yake ya Instagram, amefuta picha za Kusekwa na zile walizowahi kupiga wote kwa pamoja. Kitendo hiki amegoma kukizungumzia.

MBASH 02

Emmanuel Mbasha

Wiki moja iliyopita, Mbasha aliziibua tena tetesi za kuvunjika kwa ndoa ya Flora na Kusekwa na  utata ulizidi baada ya Flora kufuta picha.

Awali Mbasha alitangaza wawili hao wameachana, ikiwa ni mara ya pili kwake kutangaza hili na aliandika hivi kwenye ukurasa wake  wa Instagram.

“Haya jamani niliwaambia watu walishaachana muda sana ndoa imeishakufa kila mtu na hamsini zake, watu wakabisha mbona wamepostiana wamewishina birthday .. sasa mwanamke alikuwa anafanya siri watu wasijue mwanamume akamwambia FUTA picha yangu sitaki unafiki .. wameisha achana na sasaivi wako mahakamani kwenye talaka na kulea watoto mwanaume atunze watoto...

Picha zote kwenye mitandao yake ya kijamii flora kafuta alizokuwa na mmewe au ex....mpaka hapa ndoa 4 zishamshinda ikiwemo yangu..walijuaga kunipakazia haki Tena ila MUNGU NI MUNGU sio asumaniiiiii.”

Baada ya kuandika hayo, Mbasha alipata komenti nyingi sana ambazo asilimia kubwa zikimwambia ameshindwa ‘kumove on’ kwa Flora ndiyo maana wakati anamtajataja na kumposti kwa peji yake.

Wapo waliosema anatamani Flora arudishe mahusiano kwake, kwani amekuwa anamfatilia sana kwa kila kitu anachofanya na kukianika Instagram yake.

MBASH 01

Mwanaspoti lilimtafuta Mbasha

Baada ya kuona hivyo, Mwanaspoti lilimtafuta Emmanuel Mbasha ili kufahamu kwa nini  amekuwa akitangaza aliyekuwa mke wake hayupo kwenye ndoa.

“Sasa kwani ni siri jamani, (kicheko) embu niache bana na kuna bomu lingine nitaliandika, (kicheko), ndiyo muyaone sasa mimi nilisingiziwa sana nikaonekana ni tatizo,” alisema Mbasha.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilimuuliza kama anatamani kurudiana na Flora, Mbasha alicheka tu na kukata simu.