Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dude awachana Bongo Movie

Muktasari:

  • Dude aliyewahi kupita katika makundi kadhaa ya sanaa kabla ya kujitosa kwenye filamu na tamthilia alisema wasanii wa filamu waelewe, kuna wakati utahitaji msaada wa Bongo Fleva ukashindwa kupata kwa sababu uliendekeza pesa nyingi kuliko utu.

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu, Kulwa Kikumba 'Dude' amewachana wasanii wenzake wa Bongo Movie wasiendekeze sana pesa wanapotafutwa na wasanii wa Bongo Fleva ili kuzinogesha video za nyimbo zao.

Dude aliyewahi kupita katika makundi kadhaa ya sanaa kabla ya kujitosa kwenye filamu na tamthilia alisema wasanii wa filamu waelewe, kuna wakati utahitaji msaada wa Bongo Fleva ukashindwa kupata kwa sababu uliendekeza pesa nyingi kuliko utu.

"Sisi wasanii tufahamu sanaa zetu zinategemeana, hivyo utakuta msanii wa Bongo Fleva anataka kufanya video ya wimbo wake, anamtafuta msanii wa Bongo Movie anatajiwa bei kubwa sana ama anaringia kwa kuwazungusha. Sasa hii tujue, ipo siku na sisi tutawahitaji hawa watu kwa msaada, hivyo tujaribu kuendana nao sawa tu," alisema Dude.

Dude aliongeza; "Mimi binafsi nawaheshimu sana wasanii wote wa Tanzania na hata wakija kunifata kusaidia jambo huwa naangalia utu mbele halafu mengine yanafuafa, sababu hata mimi huwa nafanya kazi zangu nyingi tu na kuna kazi nyingine zinatakiwa wasanii Bongo Fleva wawepo, hivyo napata urahisi sana kwao kutokana na ushirikiano nao mzuri."