Diamond, Harmonize wamvuta Superstar M.E Tanzania

Sunday July 31 2022
super pic
By Mwandishi Wetu

Mkali wa Afropop kutoka nchini Afrika Kusini, Uwakina Emmanuel maarufu Superstar M.E anayetamba na wimbo wa Oginig amesema katika ziara yake ya kimuziki bara la Afrika atakanyaga ardhi ya Tanzania kukutana na Diamond Platnumz.

Superstar M.E ambaye pia ni miongoni mwa wasanii waanzilishi wa mdundo wa Afropiano amesema lengo la ziara hiyo ni kujitangaza na kufanya kazi na wasanii wakubwa nchi mbalimbali.

super pic 1

“Moja ya malengo yangu ni kufanya kazi na wasanii wa Tanzania, nitafanya wimbo na Diamond Platnumz karibuni pia na Harmonize ili kupata hit za kimataifa,” amesema Superstar M.E

Msanii huyo mwenye asili ya Nigeria ila ameweka maskani yake Afrika Kusini mbali na kuimba pia amekuwa mtayarishaji aliyefanya kazi na wasanii mbalimbali wakiwemo Teni, Emtee, Zahara amesema ataanza ziara hiyo nchini Namibia Agosti 6.

“Nikitoka Namibia nitaenda Zimbabwe, Msumbiji alafu Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Ghana kisha nitaenda Uingereza,”

Advertisement
Advertisement