Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dada wa MC Pilipili azungumza, majonzi yakitawala mtaani Dodoma

MC Pict

Muktasari:

  • ‎Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu Mc Pilipili, alikwenda Dodoma kwa ajili ya kusherehesha harusi iliyokuwa ifanyike jana jumapili, lakini alikutwa na umauti na sababu za kifo chake bado hazijawekwa bayana.

Vilio, simanzi na majonzi vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa mchekeshaji na mshereheshaji wa shughuli mbalimbali nchini marehemu Emmanuel Mathias (MC Pilipili) kufuatia kifo chake kilichotokea ghafla jana mchana jijini Dodoma.

‎Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu Mc Pilipili, alikwenda Dodoma kwa ajili ya kusherehesha harusi iliyokuwa ifanyike jana jumapili, lakini alikutwa na umauti na sababu za kifo chake bado hazijawekwa bayana.

‎Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumatatu, Novemba 17, 2025, nyumbani kwao Swaswa jijini Dodoma, dada wa marehemu, Veronica Mathias amesema alipata taarifa za kifo cha ghafla cha kaka yake baada ya kupigiwa simu na kaka yao mkubwa anayeishi Dar es Salaam.

M 01

‎Amesema baada ya kupata taarifa hizo alikwenda nyumbani kwao ili kujua kama taarifa hizo ni kweli na alipofika alikuta ni za kweli.

‎"Kwa kweli sijui ni nini kimempata kaka yangu mpaka kifo kikamkuta. Imekuwa ni ghafla mno kuna ndugu yetu mmoja aliyeuona mwili wake amesema ulikuwa na madoa meusi mgongoni yanayoonekana kuwa ni majeraha," amesema Veronica.

‎Amesema mpaka sasa hawajui maziko yatakuwa lini kwani bado wanamsubiri kaka yao mkubwa kutoka Dar es salaam kwa ajili ya kupanga siku ya mazishi.

‎Kuhusu mke wa marehemu na mtoto kuhudhuria msibani, Veronica amesema hawana mawasiliano nao na mpaka sasa bado hawajafika Dodoma msibani.

‎Naye mwenyekiti wa kamati ya maafa Mtaa wa Swaswa, Pascal Maingu amesema msiba wa MC huyo umeshtua wakazi wa eneo hilio kutokana na maisha waliyokuwa wanaishi na mshereheshaji huyo.

M 02

‎"Alikuwa ni kijana mzuri mchangamfu na mwenye upendo kwa majirani zake. Alikuwa akifika hapa nyumbani ni lazima apite nyumba kwa nyumba kuwasalimia na kuwachekesha kama ilivyokuwa kawaida yake," amesema Maingu.

‎Amesema taratibu za mazishi zinasubiri vikao vya ndugu ili wapange siku ya mazishi na kwamba mwili bado upo chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.