Corona yatibua Pambana la Fury na Wilder

Muktasari:

PAMBANO la ngumi kwa uzito wa juu baina ya Muingereza, Tyson Fury na Mmarekani Deontay Wilder ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika Julai 24 mwaka huu limesogezwa mbele hadi Oktoba 9 mwaka huu baada ya Bondia Tyson Fury kupimwa na kukutwa na Maambukizi ya virusi vya Corona.

BY DAUDI ELIBAHATI

Baada ya kupata maambukizi hayo bondia huyo kupata Maambukizi hayo anatarajiwa kupokea dosi ya chanjo na kutarajiwa pia kupata ya pili kabla ya pambano hilo kufanyika katika ukumbi wa T-Mobile Arena, Las Vegas Nchini Marekani.

Fury atakuwa anatetea taji lake la WBC uzito wa juu baada ya kumshinda kwa TKO Deontay Wilder katika pambano lililopita lililofanyiaka Mwezi Februari 22 mwaka jana kufuatia kutoa droo kwenye pambano la kwanza lililofanyika Desemba 1, 2018.

Tiketi ambazo zilipangwa kutumika Julai 24 zitaandaliwa upya kwa tarehe iliyopangwa ya Oktoba 9.

Fury alisema kuwa " Sina la kufanya zaidi ya kutumia dozi kwa sasa, ila matumaini yangu ni kufanya vizuri katika pambano hilo na kuhakikisha sifanyi makosa nitakaporejea imara zaidi ya hapa nilipo"

kwa upande wa Meneja wa Wilder, Shelly Finkel alisema kuwa "Bondia wangu yupo tayari kwa ajili ya kuchukua taji hilo kubwa la Dunia mwezi Oktoba"