Chuchu Hans kumzalia Ray watoto pacha

Muktasari:
- Chuchu alisema hayo mara baada ya mwanaye Jaden kutimiza mwaka mmoja, akifichua kuwa baada ya kumpatia Ray mtoto huyo, anatamani amzalie tena mapacha ili awe na jumla ya watoto wanne ndio apumzike,
STAA wa Filamu Bongo, Chuchu Hans, amedai kuwa ana mpango wa kumzalia mzazi mwenzake Ray Kigosi watoto mapacha ili atulie kama maji kwenye mtungi.
Chuchu alisema hayo mara baada ya mwanaye Jaden kutimiza mwaka mmoja, akifichua kuwa baada ya kumpatia Ray mtoto huyo, anatamani amzalie tena mapacha ili awe na jumla ya watoto wanne ndio apumzike,
Mwingizaji huyo mwenye mvuto wa kipekee ana mtoto mwingine aliyempata kwa mwanaume mwingine kabla ya kuwa na Ray.
“Baada ya kumzalia Ray mtoto kwa sasa nataka niongeze uzao mmoja wa pacha ili niwe na wanne kisha nitapumzika,” alisema Chuchu Hans.