Chid Benz atumia wiki mbili kuandaa albamu

Tuesday November 30 2021
Chid PIC
By Nasra Abdallah

Msanii wa hiphop, Rashid Makwiro maarufu Chid Benz amesema ametumia wiki mbili kuanda albumu yake mpya ya 'Watu wangu' ambayo ameitangaza rasmi leo Jumanne Novemba 30, 201.

Albamu hiyo yenye nyimbo 18 aliitumia siku nane kuandaa mashairi huku taratibu za kurekodi pamoja na mambo mengine zikichukua wiki mbili.

'Watu wangu' itakuwa albamu ya tatu kuiachia tangu alipoanza muziki huku akiomba ushirikiano kutoka kwa mashabiki zake huku akisisitiza kuwa alidondoka lakini sasa ameamua kunyanyuka na kuangalia soko linataka nini.

"Hapo katikati mnajua nilipitia changamoto mbalimbali hivyo hii ni albamu yangu ya tatu tangu miaka kumi imepita, ukiacha ile ya Chid Benzi na Dar es Salaam Stand Up, nahitaji sana sapoti ya watu ili niweze kuendelea," amesema Chid.

Kuhusu ni nani nani aliowashirikisha kwenye albamu hiyo, amesema ni wasanii wanne akiwemo Baddest 47, na wengine watatu wanaotoka kwenye kundi la 'La Familiar'.

Amesema sababu ya kutowashirikisha wasanii wengi kama wanavyofanya wasanii wengine kwenye albamu zao ni kutaka kuonekana kuna watu walimbeba bali ametaka kudhihirisha kuwa bado kipaji chake kipo palepale na kuongeza kuwa atafanya hivyo kwenye albamu ijayo anayotarajia kuiachia mwaka ujao.

Advertisement