Chege atinga na farasi

Sunday August 29 2021
chege pic
By Thomas Ng'itu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chege Chigunda ametinga uwanja wa Benjamin Mkapa akiwa na farasi.

Chege alitinga na muonekano huo katika tukio cha kilele cha wiki ya Mwananchi na alifanya shoo kwa kutumbuiza nyimbo ambazo hazikuzidi tano.

Kabla ya kuanza shoo yake aliingia akiwa na farasi na kuzunguka nae uwanja wote kabla ya kwenda kupanda katika jukwaa.

Miongoni mwa shoo ambayo alifanya vizuri ni hiyo ya Chege ambayo mashabiki wengi walikuwa wanaimba nae kwa pamoja.

Advertisement