Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cardi B ameyatimba kwa Diggs?

CARD Pict

Muktasari:

  • Uhusiano wa Cardi B na Diggs ulianza kama uvumi Oktoba 2024, ingawa Cardi B alikanusha mara kadhaa. Hata hivyo, mashabiki waligundua picha na video mbalimbali zilizowaonyesha wawili hao pamoja, na kuanza kushuku kuwa kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi kati yao.

KINACHOTIKISA duniani kwa sasa ni penzi la rapa maarufu wa Marekani, Cardi B na nyota wa NFL, Stefon Diggs, uhusiano ambao unavuma na kushika vichwa mbalimbali vya habari huku mashabiki wakisema mrembo huyo ameyatimba baada ya kumkimbia aliyekuwa mumewe, rapa Offset, kwa tuhuma za usaliti na kutua kwa mwanaume ambaye tayari ameanza kuandamwa na tuhuma za usaliti na kuzaa na mwanamke mwingine.

Uhusiano wa Cardi B na Diggs ulianza kama uvumi Oktoba 2024, ingawa Cardi B alikanusha mara kadhaa. Hata hivyo, mashabiki waligundua picha na video mbalimbali zilizowaonyesha wawili hao pamoja, na kuanza kushuku kuwa kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi kati yao.

Tetesi zilianza kushika kasi zaidi baada ya Cardi B kuachana rasmi na Offset, mumewe wa zamani.

Mnamo Mei 2025, uvumi huo ulithibitishwa wazi pale walipoonekana wakifurahia pamoja kwenye mchezo wa mpira wa kikapu huku Cardi akionekana akimkumbatia na kumbusu Diggs kwenye skrini kubwa ya ukumbi.

Miezi michache baadaye, wawili hao walitangaza uhusiano wao rasmi kupitia Instagram, jambo lililowashangaza mashabiki wengi kwani hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Cardi kutangaza hadharani uhusiano mpya tangu alipotalikiana na Offset mwezi Julai 2024.

Cardi B, ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano maarufu na rapa Tommy Jeez kabla ya kuwa na Offset, alionyesha kuwa yuko tayari kuanza ukurasa mpya wa maisha yake.

CAR 01

Cardi B na Offset walidumu kwenye ndoa yao kwa takribani miaka saba, walianza kuchumbiana mwaka 2017 na baadaye kufunga ndoa ya kimya Septemba mwaka huohuo.

Katika kipindi chote hicho walipata watoto watatu, hata hivyo, ndoa yao ilikumbwa na changamoto nyingi za misukosuko na mwaka 2024 wakaamua kuachana.

Chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ilidaiwa kuwa tuhuma za usaliti, Offset mara kadhaa alihusishwa na kashfa za usaliti, ingawa Cardi B aliwahi kumsamehe, hali hii iliendelea kuleta mizozo ndani ya ndoa.

Ukiachana na usaliti, kwa mujibu wa mahojiano ya rapa huyo, walikuwa wanagombana mara kwa mara kuhusu majukumu ya kifamilia na malezi ya watoto, ikiwamo madai kwamba Offset hakushiriki ipasavyo katika kugharamia na kulea watoto.

Aliachana na Offset na sasa yupo na Diggs, penzi lao lina mwaka mmoja, na kando na furaha ya mapenzi, wamefurahia pia baraka ya kutarajia mtoto wao wa kwanza pamoja ingawa kila mmoja tayari ana watoto kutokana na mahusiano ya awali.

CAR 02

Katika makala hii, Mwanaspoti inakuletea kwa kina matukio muhimu ya safari ya mapenzi ya Cardi B na Diggs, kuanzia uvumi hadi sasa wanapotarajia mtoto.


OKTOBA 2024

Oktoba 9 tetesi za uhusiano wao zilianza kuibuka mashabiki wakidai kuwaona pamoja maeneo tofauti.

Cardi B alikanusha kupitia Instagram Live, akisema "Mtandao huu ni kichaa kabisa hizi tetesi zote ni za ajabu sana ndiyo maana sitaki kuzijibu kwa sababu nahisi ni kama utani."


DESEMBA 2024

Desemba 18, Cardi B alikiri kuwa yupo kwenye uhusiano na Diggs, akijibu shutuma kutoka kwa Offset aliyedai kuwa anajali wanaume wengine.

Cardi alimjibu vikali Offset kwa kusema “Kwa sababu nimepata mchumba, kwa vile mimi ni single, inamaanisha najali tu kuhusu wanaume, saini hizo karatasi haraka.”

CAR 03

FEBRUARI 2025

Februari 14, Siku ya Wapendanao, Cardi na Diggs walionekana hadharani kwa mara ya kwanza, wakiingia kwenye hoteli moja huko Miami usiku wa manane.

Chaneli ya TMZ ilithibitisha tukio hilo kwa kuonyesha video yao pamoja.


APRILI 2025

Aprili 13 mastaa hao walionekana kwenye tamasha la Coachella huko California walicheza kwa furaha na kuonekana wakiwa kwenye penzi zito.

Shabiki mmoja aliandika kwenye mtandao wa X kuwa Offset huenda alikuwa akiumia moyoni. Hata hivyo, Offset alijibu kwa kusema hafanyi hivyo bali anafurahia kuona mama wa watoto wake akiwa na furaha.


MEI 2025

Tukio la kwanza, walihudhuria Met Gala, kila mmoja akiingia peke yake. Hata hivyo, walionekana pamoja baada ya tukio hilo kuisha.

CAR 04
CAR 04

Tukio la pili: Walionekana Madison Square Garden, New York, wakishangilia mechi kati ya New York Knicks na Celtics, waliingia na kutoka uwanjani wakiwa wameshikana mikono, kitendo kilichothibitisha uhusiano wao zaidi kwa umma.


JUNI 2025

Cardi B aliweka wazi rasmi kuwa yupo kwenye uhusiano na Diggs. Kupitia Instagram aliposti picha wakiwa kwenye boti wakiwa wamekumbatiana na kuongeza video ya kimahaba.


SEPTEMBA 2025

Septemba 17 Cardi B alitangaza kuwa ni mjamzito wakati akiwa kwenye kipindi cha CBS Mornings, alipokuwa akizindua albamu yake mpya Am I the Drama?


Alisema: "Ndiyo, mimi ni mjamzito. (Tumboni) Ninamlea mtoto na mpenzi wangu Stefon Diggs, nimefurahi najisikia niko sehemu nzuri. Najisikia mwenye nguvu mimi na mpenzi wangu tunasaidiana sana.”


UTATA MPYA

Wakati wawili hao wakitarajia mtoto kuna tetesi zimezuka kwamba Diggs ana watoto wengine, mbali na bintiye mmoja anayefahamika.

TMZ ilipata video ikimuonyesha Diggs akitoka hospitalini akiwa na kibebeo cha mtoto, ikidaiwa kuwa ilichukuliwa muda mfupi baada ya kutangaza uhusiano wake na rapa huyo.

Mbaya zaidi, siku moja baada ya Cardi kutangaza ujauzito wake, Diggs alipokea kesi ya uthibitisho wa uzazi kutoka kwa mwanamitindo Aileen Lopera, aliyewasilisha ombi 2024 akidai mchezaji huyo alipe gharama za kujifungua pamoja na ada za wakili, lakini Diggs alijibu hakuwa na uhakika kama mtoto huyo ni wake.

Kwa upande wake, Cardi B ameonekana kutojali tetesi hizo. Kupitia Instagram Live yake, rapa huyo alitania mashabiki waliokuwa wanatuma ujumbe wakimuonea huruma wakidai ameruka mkojo na kukanyaga kinyesi.

"Halo Barbara, Hi Shirley. Huyo ni baba wa mtoto wako? Basi huyo ni baba wa mtoto wangu pia. Sasa tufanyeje, hata sijui, tutajua tu," alisema Cardi kwa furaha.

Kuhusu mtoto wa Lopera, Diggs ameomba kipimo cha DNA kuthibitisha kama kweli yeye ndiye baba akisema endapo matokeo yataonyesha ni wake yuko tayari kumlea mtoto huyo pamoja na kushiriki kugharamia mahitaji ya mtoto pamoja na ada za kisheria.

Pia Mwanamitindo wa Instagram, Skymarlenee amelizua baada ya kudai amekuwa akitoka kimapenzi na Diggs, miezi kadhaa tangu staa huyo atangaze kuwa katika uhusiano na Cardi B.

Skymarlenee ameposti meseji na sauti alizodai alikuwa akichati na Diggs na malumbano yaliyozuka kati yake na Cardi B baada ya rapa huyo kumfumania yeye (Skymarlenee) akiwa na Diggs.

CAR 05

KAZI ZAKE

Cardi B ametoa ngoma nyingi zilizofanya vizuri kimataifa na kumpa umaarufu mkubwa, miongoni mwa ngoma hizo ni Bodak Yellow (2017), ndiyo nyimbo iliyompa umaarufu wa kimataifa, ilishika hadi nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 akawa rapa wa kwanza mwanamke baada ya Lauryn Hill (1998) kufanikisha hilo kama msanii wa Solo.


Licha ya kuteuliwa kuwania mara 10 kwenye tuzo za Grammy lakini rapa huyo alipata tuzo moja mwaka 2019 kupitia albamu yake ya kwanza 'Invasion of Privacy' kwenye kipengele cha Best Rap Album.


Mbali na tuzo hizo kubwa za muziki lakini amewahi kushinda MTV Video Music Awards (VMAs) mara nne, MTV Europe Music Awards (EMAs) mara mbili tangu aanze sanaa yake mwaka 2015.