Bendi tano za dansi kukiwasha Usiku wa Wafia Dansi' Dar

Dar es Salaam. Bendi tano za muziki wa dansi zinatarajia kuoshamvulia jukwaa moja katika tamasha la 'Usiku wa Wafia Dansi'.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Mei 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Gwambina, jijini humo.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 11,2022, Mratibu wa tamasha hilo, Bernard James kutoka kampuni ya Cheza Kidansi Entertainment ambao ndiyo wadhamini anesema lengo la tamasha hilo ni kurudisha upya muziki huo.

James amezitaja bendi hizo kuwa ni bendi ni Msondo Ngoma Music Band, Bogoss Music chini ya Nyoshi el Sadaat na Mapacha Music Band ya Jose Mara ambazo zote zinatokea Dar es Salaam.

Aidha amesema kutakuwa bendi mbili kutoka nje ya Dar es Salaam ikiwe.o Waluguru Original ya Morogoro na Mjengoni Classic ya Arusha.

"Muziki huu una idadi kubwa ya mashabiki hivyo wajibu kuendelezwa ili vizazi vijavyo viweze kufahamu nyimbo zenye ujumbe nzuri na maadili ya nchi yetu, " amesema James.

Kwa upande wake Mwimbaji wa bendi ya Mapacha Music Band, Jose Mara amesema amejipanga vizuri kutoa burudani nzuri kwa mashabiki zake na wadau wa muziki huo na kuahidi siku hiyo atazindua nyimbo zake mpya ziitwazo ' Nitakuwa Sawa' na 'Hukumu ya Mapenzi'.

Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Mo Green International ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Kessa Mwambeleko alitoa wito kwa wadau wa muziki huo kujitokeza kwa wingi kusapoti muziki wa dansi ili kurudi kama hapo awali.