Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ben Pol: Kamera zinaficha mengi nyuma yetu

Muktasari:

  • Nyuma ya Kamera na Olipa Assa, wiki hii imepiga stori na msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama Moyo Mashine, Nyumbani, Wapo na msilolijua kuhusu yeye ni licha ya kujulikana na DM za warembo katika mitandao yake ya kijamii, lakini anapata ugumu wa kumpata mtu sahihi.

TABASAMU zinazoonyeshwa na watu maarufu wanapokuwa mbele ya kamera, kuna wakati mwingine haziendani na maisha halisi ya kila siku wanapokuwa wenyewe.

Nyuma ya Kamera na Olipa Assa, wiki hii imepiga stori na msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama Moyo Mashine, Nyumbani, Wapo na msilolijua kuhusu yeye ni licha ya kujulikana na DM za warembo katika mitandao yake ya kijamii, lakini anapata ugumu wa kumpata mtu sahihi.

Ben Pol anaelezea namna ambavyo mapenzi yaliwahi kumpeleka resi, akajikuta anapata msongo wa mawazo na aliyemsaidia kukaa sawa ni Aunt Sadaka Mtaalamu wa Afya ya Akili.

Kisa cha kufikia hatua hiyo anakitaja alizama katika penzi la mrembo mmoja, walikuwa wanaishi majiji tofauti hapa nchini, alikuwa akimkosea mara kwa mara, ilifikia kipindi akaamua kuyatoroka mapenzi hayo licha ya moyo wake kuumia.

"Nakumbuka ilikuwa asubuhi moja nikasema sihitaji tena mahusiano haya, sikutaka kujua kwa upande wake itakuaje, nikazima simu na hakuna ndugu wala rafiki alikuwa ananipata, kilichonisaidia ni kuishi tofauti," anasema na kuongeza;

"Baada ya kukaa kwa muda mrefu nikawasha simu cha ajabu yule mwanamke badala ya aniombe msamaha alinitumia ujumbe wa matusi mazito, nikaona nilifanya uamuzi sahihi ya kuyatoroka, maana angekuwa na heshima angeniomba msamaha, maneno ya watu mitandaoni hayaniumizi, maana unaweza ukaposti mtu wako wanaanza kukuita kibenti, unaposti mzungu wako wanakuita huyu jamaa anapenda mtelezo na hawajui ana pesa au la, hivyo vinanisumbua kwa muda mfupi tofauti na akutukane mtu ambaye uliwekeza hisia kwake, ulilala na kuamka naye, ulifanya ubunifu wa kumpa zawadi, kumpeleka sehemu anazopenda, kumpa atensheni hiyo inauma hadi kwenye mifupa."

Anasema asilimia kubwa ya wanawake wanaowataka wanamuziki, wanakuwa na picha ya mashairi wanayoyaimba na hawapo tayari kuwabeba kama walivyo.

"Wanamuziki wengi hata wale wa nje wanasumbuliwa na mahusiano ya kweli,wasichana wengi hawaji kumpenda Ben Pol, bali wanakuwa wamenibeba katika picha ya mashairi, sasa ninapokuwa na ratiba ya kuamka asubuhi mazoezi, kushinda studio kurekodi anaona humpi atensheni."

Anaongeza: "Changamoto nyingine kubwa ambayo ilikuwa inatufanya tugombane nikiwa na ratiba za kikazi mfano nimealikwa kwenda kupafomu, naye anaanza kupanga ratiba anataka kwenda visiwani kutembea, hivyo nilikuwa naacha vyote nafanya vyake, bado akawa anataka muda wote nifanye hivyo.

"Jambo ambalo unajikuta unakaa muda mrefu bila kurekodi, unapunguza mahusiano na wasanii wenzako, maproduza, unatumia muda pesa, kifupi anakufilisi mawazo unabakia kama roboti, baadaye unakuwa mtu wa ajabu, mwenye hasira na huzuni."

Takribani miaka minne nyuma, Ben Pol aliachana na aliyekuwa mkewe Anerlisa ambaye ni raia wa Kenya, anafunguka kilichokuwa nyuma ya hilo:"Sababu kubwa tofauti na zile zilikuwa zinazozungumzwa mitandaoni, tulikuwa watu wawili tofauti, wenye misingi tofauti ya malezi, ingawa sitaingia kiundani kuelezea kila mtu ana maisha yake."

Anaulizwa kipindi hicho hicho, ulionekana umebadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu na hilo lipoje maana hukuwahi kuliongelea? Anajibu:"Ngoja nilijibu kwa mara ya kwanza katika gazeti hili,  kwa sasa nikikaa chini nikiangalia video za matukio yangu najiuliza huyo kijana Ben Pol wa hivi alikuwa na shida gani, alikumbwa na nini, mbona alikuwa mtu wa ajabu kupita kiasi.

Anaongeza: "Bahati mbaya zaidi watu maarufu tunafanya makosa mbele ya vyombo vya Habari, lakini nilijibu kwa hekima bila kuingia kiundani, naheshimu dini zote, nina ndugu zangu Waislamu na Wakristo, nashirikiana nao kwa namna yao na kwa heshima kubwa, ila mimi ninavyosali acha iwe siri yangu na Mungu."

Anaulizwa tena je, ukitaka kuoa utafunga ndoa na dini gani: "Itategemeana na mwanamke nitaendana naye kiasi gani, nitazingatia upendo wa kweli, nikijiridhisha na hilo basi nitafunga kivyovyote na uzuri mama yangu mzazi ananiamini anajua nina maamuzi ya busara.

"Mfano unakuta umetoka na mwanamke mmeenda kupata lanchi ama dina, mhudumu akachanganya kuleta mlichomuagiza, mtu anaenda kwa meneja ili afukuzwe wakati kibinadamu unaona ni kitu cha kawaida”