Baba Levo kununua nyumba ya Harmonize

Sunday May 02 2021
Baba levo pc
By Nasra Abdallah

Msanii wa vichekesho na muziki, Clayton Chipando maarufu baba Levo amesema yupo mbioni kununua nyumba aliyekuwa anaishi msanii Harmonize.

Baba Levo ameyasema hayo jana Jumamosi Mei Mosi, aliposhiriki shughuli ya kufuturisha wafanyabishara iliyoandaliwa na kampuni usafirishaji ya Silent Ocean.

Msanii huyo alisema nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kunduchi, Diamond aliimpa Harmonize aishi wakati akiwa chini ya lebo ya Wasafi.

"Yaani nimeshamuambia bosi Diamond namna naitamani hiyo nyumba ya Diamond na nia yangu ya kuinunua,kwani nshaanza kusichaanga,naamini atainiuzia na mimi nikapigwe na upepo wa baharini," amesema.

Hata hivyo, msanii huyu amesema anipa moyo kwamba atauziwa nyumba hiyo kwa kuwa ukweli ni kwamba Diamond ana nyumba nyingi na kutaja idadi yake kuwa ni 121.

Pia amesema wakati watu wakimdhihaki mkali huyo wa kibao cha Waah! Kuwa anaishi nyumba ya kupanga, ukweli ni kwamba ukiachia mbali nyumba anazomiliki,pia anajenga nyumba ya maana ambayo anaamini msanii yeyote Tanzania itamchukua miaka 60 kuijenga kama hiyo.

Advertisement
Advertisement