Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Albamu mpya ya Bruce Melodie  gumzo

Bruce Pict

Muktasari:

  • Katika albamu hiyo yenye nyimbo 21 kibao cha “Beauty on Fire”, ndicho kinachotamba zaidi ambapo alikitoa awali akiwa anaisafishia njia albamu hiyo.

STAA mahiri wa muziki wa Rwanda, Bruce Melodie ameachia albamu l mpya iitwayo ‘Colorful Generation’ ambayo ni moto wa kuotea mbali na kuwa gumzo mitandaoni.

Katika albamu hiyo yenye nyimbo 21 kibao cha “Beauty on Fire”, ndicho kinachotamba zaidi ambapo alikitoa awali akiwa anaisafishia njia albamu hiyo.

Akizungumzia namna albamu ilivyopokelewa, Bruce Melodie alisema; "Albamu hii ni kwa ajili ya kizazi kipya—Gen Z, Gen Alpha. Inaonyesha ni kwa jinsi gani ni sahihi kutazama mambo kwa utofauti."

Kwenye kazi hiyo amemshirikisha mwimbaji nyota wa Nigeria anayetamba katika muziki wa Afro-Pop, Joeboy huku ikiongozwa na Bahali Ruth na J. Chretien Munezero.

Mastaa wengine walioshirikishwa katika albamu hiyo yenye mchanyato wa ladha za  Afropop, Amapiano na R&B ni pamoja na Shaggy, Blaq Diamond na Bensoul. 

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni Intro, Wallet, Oya,Beauty on Fire [feat. Joeboy], Iyo Foto [feat. Bien] Diva, Niki Minaji [feat. Blaq Diamond], Narinziko Uzagaruka, Marijuana na Ulo.

Nyingine ni Colorful Generation,   Rosa ,  Energy, Maya, Ndi Umusinzi,  Juu [feat. Bien x Bensoul], Sowe, Kuki,  Nzaguha Umugisha, Sinya na When She’s Around ß(Funga Macho) [feat. Shaggy] - Bonus Track.