STRAIKA WA MWANASPOTI : Mabadiliko Kalenda ya FIFA, KPL yana faida Kenya

Tuesday December 3 2019

Mabadiliko -Kalenda - FIFA- KPL- faida -Kenya-Soka-wachezaji-ligi kuu Kenya-Mwanasport-MwanaspotiSoka-MwanaspotiGazeti-

 

By Boniface Ambani

Kwa mda mrefu kalenda au msimu wa soka nchini Kenya ungekuwa unakaribia kuisha ama ungekuwa umeisha kufikia sasa hivi.

Ligi Kuu ilikuwa inaanza Januari inaisha Desemba. Kwa sasa msimu au kalenda ya soka nchini Kenya imebadilika. Msimu unaenda sambamba na Kalenda ya FIFA.

Kubadilisha kwa kalenda umekuja na uzuri wake pia. Nakumbuka nchini Kenya mwezi huu wa Desemba timu nyingi sana ndogo ndogo huibuka vitongojini kutengeneza mashindano yao wenyewe ndogo ndogo. Tanzania wanaita ndondo.

Shida kubwa ambayo ilikuwepo hapo awali nii, mashindano haya yalikuwa yana jaa wachezaji wanaocheza ligi kuu nchini Kenya. Kulikuwa hakuna maana kabisa.

Mashindano kama hayo ni ya kusaka vipaji vipya ambavyo vipo vijijini na vina chipuka. Lakini sasa ulikuwa unapata vijana kama hao hawapewi nafasi ya kujieleza. Klabu zote zimejaa wachezaji wanaokipiga ligi kuu Kenya, pia wachezaji wa daraja la pili. Ilikuwa vigumu sana kwa maagenti wa soka kusaka vipaji vipya.

Ukiona mchezaji mzuri, unaambiwa huyo anacheza, Gor Mahia, Tusker, AFC Leopards, Kisumu All Stars, Bandari na kadhalika. Ilikuwa inafanyika Kenya yote mzima. Lakini kwa sasa ni vyema, kisa na maana ligi kuu Kenya inaendelea, kwa hivyo wachezaji wa ligi kuu hawaezi kupata nafasi ya kuenda kucheza mechi hizo. Hapo sasa inamaana wale wachezaji wanacheza hizi mechi ni chipukizi. Wachezaji wageni wote.

Advertisement

Wachezaji hao hawana kandarasi na klabu yoyote. Ni wachezaji ambao wanataka waonekane ili waweze kupata nafasi pia wao ya kuchezaji daraja kuu Kenya.

Kwa hivyo Kalenda hii imerahisishia maagenti wa soka Kenya kusaka vipaji vipya. Vipaji ambavyo havijulikani. Mechi hizo za ndondo za Mwezi wa Desemba zimeaanza.

Kwa sasa nimepata fursa ya kutazama mechi kadhaa na nafurahishwa kuona vijana wengi, wenye talanta ya hali ya juu wakisakata ngoma safi.

Nilipojaribu kuwahoji, walisema wanafurahi sana, kwa sababu mechi kama hizi hapo awali hawakuwa wanapata nafasi ya kucheza, kisa na maana wachezaji wa ligi kuu Kenya wakiwa vijijini kwao baada ya kupewa likizo, bado walikuwa wanakuja kucheza.

Wanaitana wanakuwa wengi mno, hadi kupata nafasi tuu hawapati.

Kwa hivyo kwa Sasa wanafurahi wako na nafasi kubwa sana ya kujieleza na wanapongeza Kalenda hii iendelee hivyo hivyo. Mimi mwenyewe nina furaha saana kwa sababu nilikuwa nimechoka na ilifika wakati kutembelea mashindano hayo ikawa haina maana tena.

Haina maana umeenda kutazama vipaji alafu wachezaji ambao wako uwanjani, wengi wao unawafahamu wote, na unajua wanako cheza. Haina maana kabisa. Lakini kwa sasa, ma agenti wa soka wako na kila sabzbu ya kufurahia, na kupiga kazi zao.

Makocha pia wanao tafuta chipukizi wako na nafasi nzuri saana ya kutazama mechi hizo. Kalenda yenyewe pia imesaidia makocha na klabu nyingi saana kujua wachezaji wao wako wapi, na wanafanya nini.

Wachezaji wengi walikuwa wanaumia katika haya mashindano, wakati msimu unaanza upya wa Januari unapata hauna wachezaji kadhaa. Ilikuwa ni shida kuweza kujua mchezaji wako aliumilia wapi. Kwa sasa wanaitamani tuu na mbali.

Hawana uwezo, hawana nguvu. Inabaki ni kutii sheria. Kwa chipukizi ambao wamepata nafasi ya kujieleza, wakati wenu ndio huu. Fanyeni bidii. Shida tu kubwa mvua inapiga kote Kenya haileti shangwe.

Kubadilika kwa miyale ya jua, hali ya angaa kumeleta pia tatizo kubwa nchni. Viwanja havichezeki Kabisa. Mvua kila kona nchini Kenya na viwanja vyenyewe balaa.

Hata hivyo katachezeka tu. Nashukuru Kalenda ya FIFA, imeleta uhai fulani katika soka la mashinani na vitongoji vyake.

Advertisement