MKEKA WAKO : Man United itakwama kwa Everton

Friday February 28 2020

Man United itakwama kwa Everton,Manchester United ,Everton ,kocha Marco Silva,mashindano ya Ligi ya Europa ,

 

By Samson Mfalila mfalilasamson@gmail.com

Everton inaingia kuivaa Manchester United keshokutwa Jumapili ikiwa na kumbukumbu nzuri ya namna walivyoicharaza mabao 4-0 miezi 10 iliyopita.

Manchester United wataingia kwa tahadhari kwenye mchezo huu ikiwa siku chache baada ya kucheza mechi ya Ligi ya Europa jana.

Everton ndio inapewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mbabe kwenye mchezo huu.

Matumaini ya Everton ya kucheza mashindano ya Ligi ya Europa sio mazuri baada ya timu hiyo kulala mabao 3-2 kwa Arsenal mara ya mwisho ingawa walicheza soka ya kiwango cha juu.

Mastraika wa timu hiyo, Dominic Calvert-Lewin na Richarlison walipiga jumla ya mashuti 17 kwenye mchezo huo.

Hata hivyo, jambo jingine la kutia moyo ilikuwa kurejea uwanjani kwa kiungo Andre Gomes baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na kuumia enka.

Advertisement

Everton haijapoteza mechi nyumbani tangu kutimuliwa kwa kocha Marco Silva, ambapo wameshinda mechi nne za ligi na kutoka sare kibao.

Straika wao Richarlison yupo vizuri, ambapo amepachika mabao manne katika mechi nne zilizopita.

Kuna kila ishara kuwa Richarlison ataendeleza makali yake kwenye mechi hii.

Manchester United kwa upande wao watakuwa wanawania kushinda mechi tatu mfululizo za ligi wakati watakapoikabili Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Everton itakuwa imepania kupata ushindi baada ya kulizwa ugenini na Arsenal.

Hata hivvyo, Everton inayonolewa na mtaliano Carlo Ancelotti ilipoteza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.

Everton kwa sasa ipo kwenye nafasi ya 11 ikiwa pointi tano nyuma ya Manchester United inayokamata nafasi ya tano.

Manchester United, hata hivyo, imekuwa na wimbi zuri la ushindi baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Watford.

Hivi sasa timu hiyo ipo pointi nne nyuma ya Chelsea inayokamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Everton sasa baada ya kupoteza mchezo wao kwa Arsenal sasa itataka kudumisha rekodi yao ya kufanya vizuri mechi zao wanazocheza kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Bila shaka Manchester United itapigana kufa kupona ili kuhakikisha inapata ushindi wake.

Katika siku za karibuni, Everton imeshinda mechi tatu kati ya nne ambazo imecheza hivi karibuni katika uwanja wa nyumbani.

Staa wa Kibrazili, Richarlison, ambaye alifikisha bao la 10 msimu huu, wikiendi iliyopita, atakuwa mtu wa kuchunga.

Manchester United inaendelea kukipiga bila Marcus Rashford, ambaye ni majeruhi.

Man Utd ilicheza vizuri hivi karibuni kwa kufanikiwa kuichapa Watford mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Hata hivyo, sasa wanakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Everton, ambao wana rekodi ya kutisha nyumbani.

Everton chini ya Ancelotti wapo vizuri na tatizo la umaliziaji ndio liliwafanya washindwe kuibuka na ushindi dhidi ya Arsenal.

United wanaonekana wapo vizuri sana baada ya kufanikiwa kushinda mechi nne na kutoa sare mbili katika mashindano mbalimbali.

Ancelotti anatazamiwa kuwa na kikosi kizuri kwani baada ya Gomes kurudi uwanjani baada ya kuwa majeruhi wakati Lucas Digne na Dominic Calvert-Lewin wanatazamiwa kuwemo katika kikosi cha timu hiyo.

Bruno Fernandes anatazamiwa kuongoza safu ya kiungo ya Manchester United na Scott McTominay anaweza kupangwa.

Advertisement