Zari aliamsha zengwe la uchawi la Hamisa

Friday July 17 2020

 

By Nasra Abdallah

Mjasiriamali Zari ambaye ni mzazi mwenzake na msanii Diamond Platnumz ameanza chokochoko tena kwa Hamisa Mobeto.

Hamisa ambaye ni pia ni mzazi mwenzie na Diamond waliofanikiwa kupata naye mtoto mmoja,kipindi cha nyuma walijikuta wakirushiana vijembe mitandaoni na Zari baada ya mahusiano yake na msanii huyo anayefanya vizuri Tanzania na Africa Mashariko kuvunjika.

Kwa muda sasa wawili hao walipumzika kurushiana vijembe,lakini leo Ijumaa Julai 17,2020 ni kama Zari kaanza kumchokoza tena mwenzio.

Hii ni baada ya msanii Idriss Sultan kuweka picha inayoonyesha wapenzi walioachana wakiwa wanatumina ujumbe mfupi kwenye simu.

Hata hivyo pale mwanaume alipotaka atumiwe picha ya mtoto,mwanamke akamtumia ya kwake huku akionyesha sehemu ya makalio kama vile anayemtega kimapenzi.

Kupitia picha hiyo Idrisa ameandika"Michezo ya Zari hii".

Kutokana na ujumbe huo Zari naye akamjibu yeye hayuko hivyo, na Diamond ambaye anamuita baba T,anajua namna gani alivyo na ushirikiano kwake.

Zari alienda mbali zaidi na kumwambia Idris amtag mwenye tabia hiyo na kuhoji au anaogopa uchawi.

Wanaofuatilia stori za mastaa hao wametafsiri kuwa hilo ni dongo la Zari kwa Hamisa.

Hii ni kutokana na Septemba mwaka 2018, familia ya Diamond na Diamond mwenyewe walimtuhumu Hamisa kuwa ni uchawi.

Jambo hilo lililoteka mitandao ya kijamii lilitokea baada ya mtabibu aliyekuwa akimtibu Hamisa kuvujisha sauti ya Hamisa iliyosikika akimtaka amtengeneza Diamond ili aweze kumuoa.

Hilo lilikuja kuthibitishwa na Hamisa mwenyewe baadaye alipohojiwa na moja ya kituo cha  redio na kueleza kuwa hakuwa na nia mbaya bali alitaka kufunguliwa njia  kama kuna waliomzibia msanii huyo mkubwa kushindwa kumuoa na kuweza kulea mtoto wao.

Advertisement