Wema: Diamond mshikaji wangu, hakuna ugomvi

Friday February 21 2020

Wema: Diamond mshikaji wangu, hakuna ugomvi,Wema Sepetu, ukurasa wa kijamii wa Instagram wa Diamond, ,

 

By Nasra Abdallah

KIMWANA Wema Sepetu amesema kuwa hajajiondoa urafiki  katika ukurasa wa kijamii wa Instagram wa Diamond, bali hawakuwahi kuwa marafiki katika mtandao huo.
Wema ameyasema hayo leo Ijumaa katika hafla ya utiliaji saini kati yake na kiwanda cha rasta cha Angel kuwa balozi wa bidhaa zao.
Wema amesema suala la kutokuwa mfuasi wa Diamond kwenye mtandao huo ni makubaliano yao tangu walivyokuwa kwenye mahusiano.
Akijibu hilo amesema siku zote walizokuwa na ukaribu si yeye wala Diamond ambaye alikuwa mfuasi wa mwenzake kwa kuwa ndio maisha waliyojiwekea.
Kuhusu tetesi za kutoelewana na Diamond kwa sasa Wema amesema wapo vizuri na ni washkaji.
“Kuna wakati hata tulitaka kuwa na kipindi katika TV ya Wasafi, ambacho tungefanya kwa kushirikiana mimi, Anti Ezekiel na Zamaradi Mketema, lakini yakatokea ya kutokea kikayeyuka.
“Kama mnavyoona sasa, mimi nina App yangu ya Wema na Zamaradi  ana TV yake kila mtu anatengeza vipindi vyake huko,” amesema Wema

Advertisement