VIDEO: Sallam SK, Harmonize waibua jambo msibani

Tuesday June 30 2020

WAKATI mke wa meneja wa msanii Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, Shamsa Kombo maarufu Shammy akizikwa jana mkoani Morogoro, tukio la meneja mwingine wa msanii huyo, Sallam Ahmed Sharaff ‘Sallam SK’ kukataa mkono wa msanii Haronize msibani liliteka hisia za mazishi hayo.

Video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha Sallam akikataa mkono wa Harmonize ambaye awali alikuwa miongoni mwa wasanii wanaounda lebo ya WCB anayoisimamia na baadaye kujiengua. Harmonize alikuwa miongoni mwa mastaa walioshiriki shughuli ya mazishi ya Shamsa yaliyofanyika katika kijiji cha Mkuyuni. Msanii huyo aliachana na WCB, Agosti mwaka jana na sasa yuko kwenye lebo ya Konde Gang ambayo anaiongoza. Mbali na tukio hilo, mastaa wengi walishiriki mazishi ya Shamsa aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Advertisement