Stamina aipeleka Usiwaze kitabuni

Friday February 7 2020

Stamina aipeleka Usiwaze kitabuni,MWANAMUZIKI wa Hip Hop nchini, Bonavetura Kibogo 'Stamina' ,

 

By Rhobi Chacha

MWANAMUZIKI wa Hip Hop nchini, Bonavetura Kibogo 'Stamina' amezindua makala ya ndoa kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii, hii ni kutokana na ngoma yake ya Usiwaze aliyoitoa mwezi mmoja uliopita.  

Stamina amesema kitabu hicho kimepita kwa watu mbalimbali ikiwemo wanasaikolojia na kinaweza kusomwa na watu wa rika zote.

"Baada ya kutoa ngoma ya Usiwaze nilipata wakati mgumu watu walikuwa na maswali mengi nimeandika kitabu hiki kina majibu ya maswali yote ambayo watu walikua wanataka kujua kuhusu ndoa" amesema Stamina.

Aliongeza kuwa baada ya kutoa wimbo huo amepokea shuhuda nyingi kutoka kwa watu wakieleza wanayokutana na mambo kama hayo kwenye ndoa zao.

Alisema lengo la kutoa wimbo huo ilikuwa kutoa elimu ila siyo kueleza mambo yake ya ndani na ndoa yake ilivunjika miezi 11 kabla ya kutoa wimbo huo.

Kitabu hiki kinapatikana kwa njia ya maandishi na video kupitia mtandao wa kijamii  wa My Book.

Advertisement