Sexy Mama bila Wema ni ishu

Friday October 2 2020

 

By KELVIN KAGAMBO

LICHA ya kwamba video inayoshikilia namba za juu za ‘trendig’ katika mtandao wa YouTube kwa takriban wiki mbili mfululizo, video ya wimbo wa Sexy Mama wa Rj The Dj aliomshirkisha Lava Lava umekumbwa na swali la kwanini hawakutumika warembo halisi kwenye wimbo huo badala yake zikatumika picha kutoka Instagram.

Tuwekane sawa; wimbo wa Sexy Mama ni maalum kwa ajili ya kuwasifia wanawake warembo, na baadhi ya mashairi katika wimbo huo yanaimbwa kwa kutaja majina ya warembo maarufu Tanzania kama vile Wema Sepetu, Irene Uwoya, Elizabeth Michael na wengine, lakini kwenye video ya wimbo huo, hajaonekana mrembo hata mmoja kati ya wote waliotajwa, badala yake zimetumika picha kutoka Instagram.

Akijibu kwanini alishindwa kutumia warembo waliotajwa, mmiliki wa ngoma hiyo ambaye jina lake halisi ni Romeo Jones, amesema kile kilichofanyika kilikuwa kinaendana na wimbo ulivyokuwa unataka.

“Ukisiliza wimbo hasa verse ya kwanza ilikuwa inaongelea sana jinsi tunavyowaona warembo hawa kupitia Instagram zao, jinsi wanavyotumia filter kuongeza uzuri wao, jinsi ambavyo huwezi kupita picha zao bila ku-like, kwahiyo ilikuwa ni sahihi zaidi kutumia picha za Instagram kuliko warembo halisi.” ameeleza RJ The Deejay.

Advertisement