Nature: Natoa wimbo kulingana na matukio

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Nature amesema akiwaza watu wanataka nini ndio anatunga wimbo kugusa jamii kutokana na kitu husika.
Juma Nature amesema hatungi wimbo kwa kukurupuka ili mradi kuwaridhisha mashabiki zake, ndio maana nyimbo zake nyingi zinaendana na matukio.
"Mimi bwana huwa natunga kitu ambacho kinagusa jamiii ,nikikaa nawaza watu wanataka nini ndio natuliza akili yangu ya kutaka kutoa wimbo kwa kipindi hicho na ndio maana nyimbo zangu nyingi zinaendana na matukio" amesema
Nature amesema kuwa kipindi cha nyuma kuingia studio ilikuwa kazi, sasa hivi mambo ya teknolojia kukuwa kila sehemu kuna studio na wapo wataarishaji wengi wenye vipaji na waliosomea ndio maana  wanamuziki wamekuwa wengi na  wanafanya vizuri na kazi zao zinatoka kirahisi.
"Kwani unajua nini, zamani na sasa ni tofauti, zamani kuingia studio ilikuwa kazi sana kutokana na uchache wa studio hivyo wanamuziki wengi vipaji vyao vilikuwa vinakufa, sio kama sasahivi haya mambo ya Digital kila sehemu kuna studio na kuna watayarisha wenye vipaji na waliosomea ndio maana kuna wanamuziki wengi wanachipukia wanafanya vizuri na kazi zao zinafanyika kiurahisi" amesema Nature.
Nature amewahi kutamba na nyimbo kama Mzee wa Busara, Inaniuma Sana, Ugali, Mtoto Iddy na nyingine, amezungumzia pia bifu za wanamuziki kuwa zinatengenezwa na mapromota.
Amesema mambo hayo yapo sana nchi za Ulaya na kwamba anapenda bifu la wanamuziki Diamond Plutnumz na Ali Kiba linaongeza hamasa na ana shauri wanamuziki wengie watoke  kupitia  staili hiyo.