Mzee Majuto amefariki dunia

Thursday August 9 2018

 

By Muyonga Jumanne

Dar es Salaam. Muigizaji maarufu wa vichekesho, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia leo Agosti 8 saa 2 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.
“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,” amesema Aligaesha.
Mzee Majuto alipelekwa nchini India kwa matibabu Mei 4 na kurejea Juni 22.

Advertisement