Kala Jeremiah aibuka na 'Rafiki'

Tuesday June 02 2020
kala pic

MSANII wa muziki wa kizazi kipya hapa Nchini Kala Jeremiah, amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kupokea nyimbo yake mpya inayoitwa 'Rafiki'
Akizungumza na Mwanaspoti leo, Jeremiah anasema, wimbo huo Rafiki hauchagui rika kwani kila umri unaweza kuusikiliza kutokana na maudhui yaliyomo ndani yake.
Anasema kwa sasa kuna vitu anavikamilisha ili kuachia ngoma hiyo rasmi kwa wapenzi wake waweze kuisikiliza.
"Namshukuru Mungu mapokeo ya ngoma zangu huwa ni mazuri. Mwezi uliopita niliachia wimbo wa kuelimisha jamii juu ya Corona sasa naachia 'Rafiki' na nina nyimbo nyingi tu kilichobaki ni muda tu kuziachia," alisema Jeremiah
Anasema yeye amekuwa akiimba nyimbo za kuelimisha jamii kwa kuwa ndiyo iliyomzunguka hivyo kupitia yeye inajifunza kitu kwa kusikiliza nyimbo zake.
"Napenda sana mambo ya jamii, na ndio maana najikita sana katika jamii, hata taasisi yangu inajishughurisha na mambo ya kijamii zaidi," alisema msanii huyo.
Msanii huyu aliwahi kupongezwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kazi zake nzuri za kuelimisha jamii akikoshwa na nyimbo yake ya 'kijana'.

Advertisement