CCM kuwakutanisha tena Diamond Platnumz, Alikiba na Harmonize

Wednesday August 5 2020

 

By Nasra Abdallah

Chama cha Mapinduzi (CCM) kitawakutanisha tena wasanii Diamond Platnumz, Harmonize na Alikiba.

Ikumbukwe wakali hao Julai 11, 2020 walipata nafasi ya kupanda katika jukwaa la CCM Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Hilo limesemwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijinii Dar es Salaam.

Bila kutaja ni shughuli gani, Polepole amesema Agosti 15 kuna jambo Uwanja wa Uhuru litakalojumuisha wasanii 109.

“Atakuwepo Diamond Platnumz na kundi lake la Wasafi, Ali Kiba na kundi lake lote, atakuwepo Harmonize na kundi lake lote na bendi zetu za Tanzania Bara na Visiwani.”

Kimsingi wasanii hawa ni wasanii wote wa nchi hii na wote hawa wameimba nyimbo za Chama cha Mapinduzi.

Advertisement

“Watanzania wote wenye mapenzi mema na amani, Watanzania wote ambao wanaomini wacha kazi iendelee na mafanikio yote ya maendeleo tunataka tupige dabo, tukutane pale uwanja wa Taifa,”amesema Katibu huyo.

Wasanii wengine watakaokuwepo ni TID na 20 Percent ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu.

Advertisement