Ben Pol amleta Anerlisa kula Valentine Day Tanzania

Thursday February 13 2020

Ben Pol amleta Anerlisa kula Valentine Day Tanzania,msanii wa bongo fleva, Ben Pol, Valentine Day ,mpenzi wake Anerlisa,

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam.Februari 14, siku ya wapendanao duniani huonyeshana upendo na kupata muda wa kukaa pamoja ndicho anachotarajia kukifanya msanii wa bongo fleva, Ben Pol.

Ben Pol ameweka wazi siku hiyo itakuwa maalumu kwake kukaa faraga na mchumba wake Mkenya Anerlisa ambaye anakuja Tanzania kwa ajili ya hilo.

"Sina maana kwamba siku nyingine simpendi mchumba wangu, ila hii ni siku maalumu kama watu wanakaa na wapenzi wao duniani kwa nini yeye nisimpe nafasi ya kufurahi na mimi,"

"Atakuja hapa Tanzania, nitamwandalia mazingira ambayo atafurahia uwepo wangu nakumuimbia nyimbo mbalimbali, hiyo yote nikumuonyesha namjali kiasi gani,"amesema.

Ben Pol aliyeimba nyimbo mbalimbali zinazohusiana na ukweli wa mapenzi yake kama Ntala Naye, amesema mchumba wake ana haki ya kuimbiwa nyimbo nzuri kwa kuwa yeye ndiye chaguo lake.

"Nawashauri wasanii wenzangu kukaa karibu na wawapendao iwe wazazi, watoto, wake ama marafiki, inakuwa inapendeza kwani mnakuwa mnapata wasaa mzuri wakujuana zaidi," amesema Ben Pol.

Advertisement

Advertisement