Tamasha la Sauti za Busara kuwaenzi Ruge, Faki Makame

Muktasari:

Tamasha la 17 la Sauti za Busara limezinduliwa rasmi leo Februari 13 visiwani Zanzibar huku wakiwaenzi  wa moja wa waasisi wa tamasha hilo marehemu Ruge Mutahaba na Makame Faki Makame.

Dar es Salaam. Tamasha la 17 la Sauti za Busara limezinduliwa leo na kuwaenzi wa waasisi wa tamasha hilo marehemu Ruge Mutahaba pamoja na Makame Faki Makame katika eneo la kihistoria Ngome Kongwe, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari  visiwani Zanzibar, leo Februari 13 Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud aliwasihi Watanzania na wageni kujumuika kwa pamoja na kushuhudia kwa kushiriki katika tukio hilo la aina yake.

“Leo tunaanza tamasha hili la aina yake katika mwaka, wakati Zanzibar itakuwa inaandaa siku nne mchana na usiku bila kusimama za muziki wa kiafrika chini ya anga la Afrika, Tamasha lina majukwaa matatu na ambayo yote kwa asilimia 100 wanamuziki wotw watapiga muziki ‘live’ ikiwamo muziki utakaokuwa unapigwa bure katika bustani za Forodhani” alisema  Yusuf Mahmoud

Naye  Mwenyekiti wa bodi  ya Busara promotion,  Mohamed Simai ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu katika serikali  ya mapinduzi ya Zanzibar amesema   katika uzinduzi huu ni furaha kuona wazo la watu saba leo limekuwa wazo la watu wengi wanapata faida nalo.

"Tulianzisha tamasha hili watu saba leo hii limekua na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi jamii inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na tamasha hilo," alisema Muhamed Sumai.

Aliongeza kuwa katika timu ya watu waasisi wa tamasha hili alikuwepo marehemu Ruge Mutahaba ambae ametangulia mbele za haki pamoja na Mzee Makame Faki Makame.

Hili ni Tamasha la 17 la Sauti za Busara toka kuanzishwa kwake.