Sikia alichokisema Dora wa Kapuni

Saturday October 5 2019

 

By Olipa Assa

STAA wa kike anayetamba kwenye tamthilia ya Kapuni, Wansukura Zachael 'Dora' amesema anaamini wanarejesha heshima bongo muvi kwa kishindo baada ya kuyumba kwa muda mrefu.
Katika tamthilia ya Kapuni, Dora amecheza kama msichana anayeongea sana, mpenda haki na anafanya kazi ofisini, alisema kwa sasa jamii imeanza kuelewa kazi zao.
Alisema miaka ya nyuma jamii ilikuwa inachukulia poa kazi zao, tofauti na sasa ambapo tathilia ya kapuni na huba zinatamba na wanaona kuungwa mkono.
"Jamii ilihamia kutazama kazi za nje na ulikuwa unawasikia kazi za bongo bhana, hilo limetuasmha kufanya kazi kwa ubunifu," alisema Dora na kuongeza;
"Kwa upande wangu imeniongezea thamani na kujulikana zaidi na naona muitikio jinsi ulivyo mkubwa, tumerejesha heshima yetu kwa kishindo," alisema.

Advertisement