Ben Paul aja kibao cha Ebeneza

Friday January 24 2020

 Ben Paul aja kibao cha Ebeneza-MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Paul - kushukuru Mungu-

 

By Olipa Assa

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Paul ameachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Ebeneza huku baadhi ya mistari ikiwa ni ya kushukuru Mungu.
Ben Paul amesema kama kuna watu wanadhani amepotea kwenye gemu basi watakuwa wanachanganya mafaili akisisitiza kwamba anashukuru Mungu anaendelea kupambana na  ana nafasi kubwa sokoni.
Amesema wimbo wake wa Ebeneza umefafanua uhalisia wa anafanya nini kwenye  muziki  na kwamba amemshukuru Mungu alipomtoa mpaka alipofika.
"Sijaona cha kuniyumbisha sokoni, nitabakia kuwa Ben Paul na mwingine atabakia kuwa yeye naendelea kufanya bila presha ya kushindana na mtu sokoni,"
"Ukijua mashabiki wako wanataka nini na wewe unafanya nini sioni sababu kuumiza kichwa kukimbizana sokoni, hivyo nasisitiza kwamba bado nafanya kazi,"amesema.

Advertisement