Ben Paul afichua siri ya mrembo wa Kenya

Friday June 7 2019

 

By Olipa Assa

MAPENZI bhana sio kitu cha mchezo mchezo na ndio maana wahenga wanasema mpende anayekupenda, ndicho kilichotokea kwa msanii wa bongo fleva, Ben Paul amejikuta akiangukia kwenye penzi zito na mrembo kutoka Kenya.
Ben Paul yupo mapenzini na mwanadada anayejulikana kwa jina la Anerlisa Muigai ambaye hivi karibuni amemvisha pete ya uchumba, akitaka kumchukua mazima.
Ben Paul amefichua kitu kilichomfanya anase kwenye  penzi zito la Anerlisa kwamba ni mwanamke anayesimama kwenye nafasi yake na baada ya kuwa naye ameona umuhimu wa ndoa.
Anafunguka kuwa awali hakuwahi kufikiria kuoa licha ya kuwa kwenye mahusiano, lakini baada ya kumpata Anerlisa basi kila kitu kimebadilika.
"Sijakurupuka kuingia naye kwenye mahusiano na wala sijampendea pesa kama maneno ya watu, kuna vitu adimu ambavyo nimeviona kwake.
" Ninavyokuwa naye anajua kusimama kwenye nafasi yake, mfano anaamka mapema ananitengea chai na kuniletea kitandani, nikiingia bafuni nakuta ameishaninyooshea nguo za kuvaa.
"Mwanaume yupi hapendi mwanamke wa staili hii, ilinichukua muda kumpima tabia zake kama zinanifaa au lah, basi watu wajue hilo, mimi ni mwanaume natafuta pesa, hivyo nimempenda kwa moyo wa dhati"anasema.

Advertisement