Ben Paul: Bado nipo kwenye gemu

Tuesday December 24 2019

 

By Olipa Assa

MSANII wa Bongo Fleva, Benard Paul 'Ben Paul' amekuja na kibao kinachoitwa Sikukuu baada ya ukimya wa muda mrefu, alichosema ni maalumu kwa ajili ya mashabiki wake.

Ben Paul amesema ameamua kuwatakia kheri mashabiki wake kupitia kibao hicho, akiamini watafurahia kusikiliza burudani hiyo.

Ben Paul amesisitiza kwamba bado anazifanya kazi za muziki tofauti na watu wanavyomuona amepotea kwenye gemu.

"Nimeona nifanye uungwana wakuwapa zawadi ya wimbo mashabiki wangu ili waweze kufurahia sikukuu za Krimasi na kuvuka salama mwaka mpya,"

"Kuna mashairi nilioimba kwamba wapo wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki sisi ni nani kwa Mungu tunapaswa kushukuru, hakika ni nyimbo nzuri naamini wataifurahia," amesema.

Advertisement