Azam kupooza machungu kwa Ndanda

Muktasari:

Azam wanaingia wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga waliofungwa kwa mabao 2-1 nyumbani.

Dar es Salaam. Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC itakuwa na kibarua cha kupunguza pengo la pointi kati yao na Simba wakati watakapobiliana na Ndanda FC kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Azam Complex leo usiku.
Azam wanaingia wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga waliofungwa kwa mabao 2-1 nyumbani.
Azam yenye pointi 30, kama itashinda mchezo huo itafikisha pointi 33 na kuiongozea presha Simba kileleni pamoja na kuikimbia Yanga yenye pointi 28 kabla ya mechi yake na Lipuli leo.
Mechi nyingine leo zitakuwa kati Stand United inayoshirikia watajiuliza mbele ya Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kambage Shinyanga.
Mbao FC wataikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Kagera wanakwenda katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Mbao katika mchezo wa mzungumko wa kwanza.
Prisons inayoshika nafasi ya pili itawakaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Majimaji wataialika Mbeya City wakati Singida United watakuwa nyumbani Uwanja wa Namfua kucheza na Mwadui FC.