Bella kulianzisha mapemaaa

Thursday July 27 2017

 

By Mwandishi wetu

MASHABIKI wa muziki wa dansi wa mikao ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbela, Rukwa na Singwe wakae mkao wa kula kwani King of Melods, Christian Bella anatarajiwa kuwaibukia kuwachangamsha.

Bella na Malaika Band, wataibukia pande hizo kuanzia kesho Ijumaa akiwaimbisha zile nyimbo zilizompatia umaarufu nchini ukiwamo Nani kama Mama.

Mratibu wa ziara hiyo ya Bella na kundi lake la Malaika, Kassa Mussa alisema kuwa ziara hiyo itaanzia Mbeya kwenye Ukumbi wa City Pub, kabla ya kusogea Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, Rukwa keshokutwa Jumamosi.

“Jumapili watamaliza kazi kwa kuwasha moto High Class mjini Tunduma na kubwa ni namba Bella atakavyowachezesha sebene mashabiki wake wa mikoa hiyo ambao wana muda mrefu hawajamuona,” alisema Mussa.

Bella mwenyewe amethibitisha kwenda kuwasha moto mkoani kwa kusema wataondoka jijini Dar es Salaam leo Alhamisi wakiwa kamili, huku akiahidi kuwapa burudani ya aina yake mashabiki wake ambao wanamsubiri kwa hamu.

Mwanamuziki huyo aliyetambulishwa nchini na Akudo Impact kabla ya kuibukia Malaika Band ni kati ya waimbaji wenye kukonga nyoyo za mashabiki kutokana na tungo kali na umahiri wa kuitumia vema sauti yake kuwapa burudani mashabiki.