Wenger ashusha hasira kwa Klopp

Friday September 8 2017

 

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa  Alex Oxlade-Chamberlain alishawishiwa na Liverpool wiki moja kabla ya kumnasa kwenye siku ya mwisho ya dirisha la usajili.
 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alitua Liverpool kwa ada ya Pauni 40 milioni ikiwa ni kiasi kikubwa cha pesa kutolewa kwenye siku ya mwisho ya usajili uliopita, katika Ligi Kuu England.

Wenger anaamini Liverpool ilicheza ‘mchezo mchafu’ kwenye mechi dhidi yao ambayo ilimalizika kwa kikosi hicho cha Emirates kupata kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa kikosi cha Jurgen Klopp.
Wenger anaamini kwamba kitendo hicho kilimfanya mchezaji huyo aondoe mawazo uwanjani na huenda jambo hilo lilisababisha wale kichapo.