Waamuzi wa tenisi kupoteza ajira

Muktasari:

Kwa mara ya kwanza katika mashindano ya chama hicho kutakuwa na mwamuzi mmoja tu uwanjani, ambapo maamuzi mengine yatafanywa na teknolojia hiyo 'Hawk-Eye Live' kutambua kama mtupo upo ndani au nje.

Uingereza. Kibarua cha majaji wa pembeni katika mchezo wa tenisi sasa kitaota nyasi baada ya Chama cha Wanatenisi wa Kulipwa (ATP) kutangaza kuanza kutumia kengele za kieltroniki.
Kwa mara ya kwanza katika mashindano ya chama hicho kutakuwa na mwamuzi mmoja tu uwanjani, ambapo maamuzi mengine yatafanywa na teknolojia hiyo 'Hawk-Eye Live' kutambua kama mtupo upo ndani au nje.
Uamuzi wa teknolojia hiyo utakuwa ndio wa mwisho na wachezaji hawataruhusiwa kuupinga tofauti na walivyozoea kufanya.